Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli akipokea risala toka kwa Kaimu Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Tabora Mkuu wa gereza SSP Nahman Koko wakati yeye na mke wa
Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya
Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa mahabusu.
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi Naibu Mkuu wa gereza la
Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi wakati yeye na
mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya
mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu
leo Februari 14, 2017.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa zawadi Naibu Mkuu wa gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 201
Mke wa Rais Mama Janeth magufuli
na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akiwashukuru sana kutembelea Magereza ya
mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu
leo Februari 14, 2017
PICHA NA IKULU
……………….
NA MWANDISHI MAALUM
MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth
Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametembelea Gereza
la Mahabusu Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu
gerezani hapo.
Wake wa viongozi wametembelea
gereza hilo leo (Jumanne, Februari 14, 2017) wakiwa katika ziara
mkoani Tabora, ambapo Mama Janeth amesema wameamua kuwatembelea
wafungwa na mahabusu hao kwa nia ya kuwafariji kwa kuwa wao ni sehemu ya
jamii.
“Vitabu vitakatifu vinasema kwamba
ukiwasaidia watu wenye mahitaji utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa
Mwenyezi Mungu, hivyo tumeamua kuja kutembelea wafungwa na mahabusi
kwenye gereza hili na kuwapa zawadi kwa kuwa nanyi mnahitaji faraja,”
amesema.
Amesema wameamua kwenda kuwaona
wafungwa na mahabusu hao kwa lengo la kuwafariji na kuwatia moyo kwa
sababu wanaimani kwamba wakitoka watakuwa raia wema na hayo wanayopitia
ni sehemu ya kufanya marekebisho ya tabia.
“Ni siku kubwa kwangu, nimejifunza
mengi baada ya kufika hapa. Kitendo cha kwenda kuwaona wenye mahitaji
wakiwemo wagonjwa, wafungwa ni jambo jema tunaamini hizi zawadi
tulizozitoa zitawasaidia kwa sababu tunajua mnamahitaji mengi,” amesema.
Katika gereza hilo wake hao wa
viongozi wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu, ambapo
mwakilishi wa wafungwa hao Deo Kitave aliwashukuru kwa niaba ya wenzake.
“Tunawashukuru kwa kutukumbuka, tunamuomba Mwenyezi Mungu muendelee
kuwa na moyo huo,”.
Tags
MSAADA