BANDA MEDIA BLOG

SERENGETI BOYS KUTEMBELEA SOBER HOUSE BAGAMOYO



 Serengeti BAGA
Timu yaTaifa ya mpira wa miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka17 ‘Serengeti Boys’, Jumamosi tarehe 04 Machi, 2017, watatembelea Kituo cha vijana wanaopatiwa matibabu baada ya kuathirika na dawa za kulevya.

Kituo hicho kinachoitwa Sober House kipo Bagamoyo mkoani Pwani. Ni kituo maalumu kwa tiba ya vijana kinaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la Life and Hope Rehabilitation Centre chini ya Mkurugenzi, Al-Karim Bhanji.
Ikiwa huko, vijana wa Serengeti Boys ambao kwa sasa wako kwenye kipindi cha mabadiliko ya katika sayansi ya mwili hivyo itakuwa somo kubwa kwao katika kujielimisha kuhusu mustakabali wamaisha yao.
Kwa upande wa TFF kuwapeleka vija na hao huko ni utekelezaji Kanuniya 36 (7) ya Ligi Kuu ya Vodacom inayozungumza kukataa rushwa, madawa, ubaguzi, fujo, kamari na mambo mengine

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG