Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta wa klabu ya
KRC Genk amejikuta katika wakati mgumu usiku wa Jumanne hii wakati timu
yake ya KRC Genk ilipokuwa ikicheza na KV Oostende katika mchezo wa
kombe la Ubelgiji.
Samatta aliumia katika daika ya 23 na kulazimika kutolewa nje ya uwanja
na kumpisha Jose Naranjo ambaye alikosa p3enati katika mchezo huo.
Katika mchezo huu ambao Genk walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani
Luminus Arena walijikuta wakipoteza mchezo huo kwa kufungwa goli 1-0
dhidi ya KV Oostende na kutolewa katika kombe hilo huku goli hilo
likifungwa dakika ya nane na Knowledge Musona ambaye ni raia wa nchini
Zimbabwe.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA
