Meli ya MV. Clarias inayomilikiwa
na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), inayofanyiwa ukarabati katika
bandari ya Mwanza, ukarabati wake utakamilika mwanzoni mwa wiki ijayo na
kuanza kutoa huduma mwishoni mwa mwezi huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng.Dkt, Leonard Chamuriho,
akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli
(MSCL), Bw. Eric Hamisi (mwenye shati jeupe), wakati alipokagua
ukarabati wa Meli ya MV. Clarias.
Fundi wa Kampuni ya Huduma za
Meli (MSCL), akiendelea na ukarabati wa meli ya MV Clarias ambayo
ukarabati wake utakamilika mwishoni mwa wiki na kuanza kazi ya kutoa
huduma katika Ziwa Victoria.
Nahodha wa Meli ya Kampuni ya
Huduma za Meli (MSCL), Swedi Ruganza akitoa maelezo ya namna nahodha
anavyoendesha meli kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho (katikati),
alipofanya ukaguzi wa ukarabati wa meli hiyo jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng.Dkt. Leonard Chamuriho,
akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Huduma za Meli (MSCL), Bw.
Eric Hamisi (wa pili kutoka kushoto), mara baada ya kuangalia kina cha
maji katika bandari ya Mwanza.
PICHA NA Biseko Lisso Ibrahim, WUUM (U)
…………………………………………………………………………….
Na Biseko Lisso Ibrahim, WUUM (U)
Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya uchukuzi), Eng. Dkt. Leonard
Chamuriho ameipongeza kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL), kwa
kukarabati meli zake kwa kutumia fedha za ndani na hivyo kuhuisha
utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Akizungumza jijini Mwanza mara
baada ya kukagua huduma zinazotolewa na kampuni hiyo Eng. Dkt. Chamuriho
amesema Serikali itawekeza kikamilifu kwenye kampuni hiyo baada ya
kuridhika na utendaji uliopo sasa.
“Fanyeni kazi kwa bidii na fikra
mpya Serikali inashughulikia kwa karibu suala la mishahara yenu na
stahili nyingine” amesema Eng. Dkt. Chamuriho.
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alimteua Kaimu Meneja Mkuu
mpya wa kampuni hiyo Bw. Eric Hamisi ambaye kwa kushirikiana vema na
menejimenti na wafanyakazi wamewezesha kuongeza mapato kwa kwa asilimia
100.
Kampuni ya huduma za Meli MSCL ni
moja ya kampuni ya Meli yanayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 na
kusimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya
Uchukuzi na inatoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika
maziwa makuu yaliyopo nchini Victoria,Nyasa na Tanganyika
Tags
USAFIRISHAJI