Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema ile hali ya
polisi kuwakamata wabunge hovyo sasa mwisho baada ya jana Ndugai kutoa
uamuzi kuwa Afisa yoyote wa Serikali ambaye atakuwa akimuhitaji mbunge
ni lazima kwanza atoe taarifa kwa spika
Hali hii imefikia baada ya Jumatano bunge kupitisha azimio la kutaka
kwanza ruhusa ya spika wa bunge pale vyombo vya dola kama polisi
wanapokuwa wanamuhitaji mbunge yoyote kwa jambo lolote.
"Leo (jana) Spika wa Bunge ametoa uamuzi wa Spika kwamba Afisa wa
Serikali anapomtaka mbunge kwa jambo lolote lile lazima kwanza kupata
kibali chake. Mabunge yote ya Jumuiya ya Madola hulinda kwa wivu mkubwa
hadhi yake kama mhimili.
Sasa kukamata kamata wabunge hovyo mwisho. Lazima mihimili iheshimiane.
Sasa tuone kama Sirro atamfuata Mbunge wa Hai kama alivyosema" alisema
Zitto Kabwe
Mbali na hilo Mhe. Zitto Kabwe ametoa pongezi kwa wabunge wote pamoja na
Spika wa bunge kwa kuonyesha msimamo na kupigania heshima ya bunge
"Nawapongeza wabunge wote kwa kuonyesha msimamo katika jambo hili na
ninampongeza sana Spika Ndugai kwa kusimamia heshima ya bunge lake"
Alimalizia Zitto Kabwe
Tags
Bunge
