Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisimama Bungeni
juzi, February 10, 2017 kuzungumza vitu mbali mbali vinavyohusu wizara
yake ambapo aligusia kuhusu maswali anayokutana nayo kwamba kwanini
hajaonekana akiongelea sakata la dawa za kulevya toka limeibuka Dar es
Salaam.
Waziri Mwigulu alizungumza yafuatay:
“Lililoongelewa sana ni hili la dawa za kulevya, vita ya dawa za kulevya
ni vita ya kila Mtanzania na haijaanza sasa, mimi tangia nilipofika
nilikuta tayari Mh. Kitwanga ameshakamata Mapapa Wakubwa tu na
tulivyotoka pale tumeendeleza.
“Ninachowaambia Waheshimiwa Wabunge tunaweza kutofautiana mtazamo kwenye
approach na nyinyi kama Wabunge na Washauri wetu mkitushauri njia nzuri
za kufanikisha jambo hili sisi mara zote tutakua tunapokea ushauri huo
sababu vita hii ni yetu sote.
“Jambo moja tu ambalo nawahakikishia na ambalo nawaomba wote tuwe nalo,
tusibadili lengo… na kuna watu wengine walikua wanasema mbona Waziri
hujasema? ……..nimeshazunguka mikoa yote kasoro Njombe, Ruvuma, Singida
na Songwe, kwenye mikoa yote huko nimetoa maelekezo ya kufanyiwa kazi,
mojawapo ni dawa za kulevya.
“Nikishatoa maelezo kama hayo sibinafsishi tena hiyo shughuli, Mtanzania
ambaye inamuhusu popote alipo lazima tusimamie mambo haya kwa upana
wake, Waheshimiwa Wabunge katika maswala haya ya kitaifa tushirikiane
wote, watu huwa hawagombani kwa ajili ya kazi watu huwa wanasaidiana
kazi.” Alisema Mwigulu.
Tags
Bunge
