Baba Askofu Dr. Gwajima, ameanza mchakato wa kunua Treni ya mwendo kasi
ambayo itakua inatoka Dar hadi Morogoro. Katika usajili bado anawekewa
Zengwe, ila nia yake ni nzuri kabisa.
Katika Tanzania ya Viwanda, hatuwezi kufanikiwa Tanzania ya viwanda kama
hatuna Usafiri wa Uhakika wa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Tayari kashafanikisha Mpango wa kujenga chuo cha Urubani, anasubiri
ruksa ya Rais Magufuli. Dr Gwajima alishampeleka Mkufunzi wa mambo ya
ndege kusomea kufundisha mambo ya ndege. Kwa Tanzania watu wengi
wanapenda Urubani lakini garama za masomo ni kubwa. Hivyo kampeleka Kaka
John kusomea Ualimu wa ndege. Nadhani wote mnamjua John wa Ufufuo na
uzima. Ni kijana mwenye akili sana.
Hadi sasa Dr Gwajima kushirikiana na Msukuma(Mbunge) wameshaanza
mchakato wa kumuona Rais ili awape sehemu ya kujenga chuo cha Urubani.
Vilevile ameshaagiza Chopa tatu kwaajili ya wanafunzi.
Wito wangu
Naomba Serikali isilete siasa katika hili Swala kwani lina manufaa kwa
Watanzania. Tutawanyanyasa wawekezaji lakini Kenya ikiwachukua tunaanza
kulalamika.
Askofu Dr Gwajima kwa wasiomjua, ni Askofu wa Makanisa ya Ufufuo na
Uzima ambayo ni Zaidi ya Makanisa mia nne(400) Dunia. Vilevile ana
makampuni mengi kama makanisa mengine yalivyo na mabank mfano Mkombozi,
Efatha Bank nk.
Dr Gwajima ni Mwalimu ambaye Hulipwa zaidi ya dola 1,000/= kwa saa.
Anafundisha Mambo ya Kiroho Duniani na huwa anaalikwa kufundisha hata
kwa miezi mitatu.
Kwa sasa anamiliki ndege ambayo humuwezesha kuhudumia Ibada katika Makanisa Matatu Tofauti mikoa tofauti kwa siku.
Tags
USAFIRISHAJI
