Serikali imesema kuwa kati ya walimu zaidi ya 8,000 wa Sayansi na
Hisabati waliotajwa kuhitaji ajira serikalini, ni walimu 2100 pekee
waliotuma maombi, ikimaanisha kuwa kuna walimu zaidi ya 5,000 ambao
hawajulikani waliko.
Takwimu hiyo imetajwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na
Utawala Bora) Angela Kairuki wakati akizungumza na watumishi wa umma
wanawake katika Manispaa ya Dodoma katika wiki ya maadhimisho ya miaka
40 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kairuki alikuwa akizungumzia suala la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa
umma, na kusisitiza kuwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu watumishi wote wa
umma ambao watakuwa hawajawasilisha vyeti vyao vya kitaaluma
watafukuzwa kazi.
Amebainisha kuwa katika zoezi lililofanywa na mamlaka ya vitambulisho
vya Taifa (Nida) waligundua watumishi wengi hawana vyeti na baadhi yao
wanatumia vyeti feki hasa wa kada ya ualimu kwa kuwa wana uhakika wa
ajira pindi wanapomaliza vyuo.
"Kulikuwa na taarifa kuwa kuna zaidi ya walimu 8,000 waliokuwa
wanatakiwa kuajiriwa lakini baada ya serikali kutangaza nafasi hiyo ni
walimu 2,100 tuu ndiyo walioomba nafasi mpaka sasa.
Sasa hapo suala la kujiuliza je hao wengine mpaka sasa wako wapi kama
hawana vyeti feki!? Nataka niwaambie kuwa hakuna mwenye cheti feki
atakayesalimika kwenye Utumishi wa umma," amesema Kairuki.
Amesema ni bora aonekane ni waziri anayechukiwa na jamii kuliko kulifumbia macho suala la vyeti feki kwa watumishi wa umma.
"Tumetoa muda wa kutosha kwa watumishi wa umma kuwasilisha vyeti vyao
vya kitaaluma bila shaka walifika mpaka hapa kwenu lakini jambo la
kusikitisha ni kwamba mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi bado
hawajawasilisha," alisema Kairuki.....Vyeti hawajaleta na hata namba ya
utambulisho (index number) hawaleta sasa wanataka tuwafanyaje???
Nawamegemea tu siri na mkawaambie na wenzenu itakapofika Machi Mosi
hawajawasilisha vyeti vyao tunawafukuza kazi."
Amesema kama serikali itaharakisha zoezi hilo watumishi wa umma
wanaostahili watapandishwa vyeo na mishahara yao kwa kuwa zoezi hilo
limesitishwa kutokana na uhakiki wa vyeti.
Tags
HABARI KITAIFA
