RAIS Donald Trump wa Marekani amemkatia simu Waziri Mkuu wa Australia,
Malcolm Turnbull wakati wakizungumzia makubaliano ya nchi hizo juu ya
wakimbizi.
Mawasiliano hayo ya simu kati ya Rais Trump na Turnbull, yamezua maswali kuhusu makubaliano ya kuwachukua wakimbizi.
Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, Trump alitaja mawasiliano
hayo kuwa mabaya zaidi kati ya yale aliyoyafanya na viongozi wa dunia
siku hiyo, ambapo aliikata simu hiyo.
Bwana Trump kisha aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa atafanyaia uchunguzi makubaliano hayo.
Makubaliano hayo yaliyoafikiwa wakati wa utawala wa Rais Obama,
yatasababisha hadi watafuta hifadhi 1,250 wanaoelekea Australia kupewa
hifadhi nchini Marekani.
Australia imekataa kuwakubali wakimbizi wengi wao wakiwa ni wanaume
kutoka Iran, Afghanistan na Iraq na badala yake wamewazuilia katika
vituo vilivyvo kwenye visiwa vya Nauru na Papua New Guinea.
Waziri mkuu Turnbull amekuwa akitaka kujua hatma ya makubaliano hayo
baada ya Trump kusaini amri ya kuzuiwa kwa muda wakimbizi kutoka nchi
saba zilizo na waislamu wengi kuingia nchini Marekani.
Bwana Turnbull baadaye alsema kuwa alikasirishwa kuwa mawasiliano hayo yaliwekwa hadharani.
Alikiambia kituo kimoja cha redio mjini Sydney kuwa ripoti kwamba Trump alikata simu si za ukweli
Tags
KIMATAIFA

