Kauli ya leo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda kwamba ana uwezo wa
kumhamisha mtu yeyote kutoka kwenye Mkoa wake ni mfano mwingine wa aina
ya wanasiasa waliopewa madaraka na Rais Magufuli ambayo hata hawayaelewi
na, kwa sababu hiyo, hata wao wenyewe hawajielewi.
Nafasi ya Wakuu wa Mikoa imetambuliwa na ibara ya 61 ya Katiba yetu.
Ibara ya 61(4) inafafanua kwamba kila Mkuu wa Mkoa atatekeleza kazi na
majukumu yaliyofafanuliwa na, au chini ya, sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge.
Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili ya kufafanua kazi na majukumu ya Wakuu wa Mikoa ni Sheria ya Tawala za Mikoa ya 1997.
Sheria hiyo ndiyo iliyowapa Wakuu wa Mikoa na Wilaya mamlaka ya
kipolisi, yaani mamlaka ya kukamata watu wanaosadikiwa kufanya makosa ya
jinai mahali ambapo hakuna askari polisi.
Mamlaka haya ni madogo sana tofauti na Wakuu wa Mikoa au Wilaya wa aina ya Makonda wanavyoamini au kuaminishwa.
Kwanza, ni mamlaka ya nyongeza (supplementary powers) tu kwa mamlaka ya
Jeshi la Polisi ambalo ndilo lenye mamlaka hasa ya kukamata wahalifu.
Hii ina maana kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya hawezi kutumia mamlaka ya
kipolisi pale ambapo tayari kuna askari polisi. Polisi wanatakiwa
wafanye kazi yao bila kuamriwa na Mkuu wa Mkoa au Wilaya.
Pili, mamlaka ya kipolisi yamewekewa masharti ya muda, yaani, mtu
aliyekamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anatakiwa apelekwe
mahakamani au aachiliwe huru ndani ya muda wa masaa 48.
Tatu, Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyetoa amri ya kukamata mtu chini ya
mamlaka yake ya kipolisi, anatakiwa - haraka iwezekanavyo - kupeleka
taarifa ya maandishi kwa hakimu juu ya kukamatwa kwa mtu huyo na sababu
zake.
Sheria imeweka wazi kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya asiyetekeleza masharti
haya hataruhusiwa kumkamata mtu huyo kwa kosa hilo hilo na anaweza
kushtakiwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka yake.
Hakuna mahali popote katika Sheria ya Tawala za Mikoa ambako Mkuu wa
Mkoa au Wilaya amepewa mamlaka ya kumwondoa mtu yeyote kwenye Mkoa au
Wilaya yake.
Mamlaka ya kuondoa watu kwenye maeneo yao, yaani deportation, yalikuwa
sehemu ya mamlaka ya Rais kwa mujibu wa Sheria ya Kuondoa Watu
(Deportation Ordinance).
Sheria hii ya kikoloni ilitangazwa kuwa kinyume na Katiba, na kwa hiyo
batili, na Jaji James Mwalusanya wa Mahakama Kuu katika kesi maarufu ya
Chumchua Marwa na Wenzake ya mwaka 1987.
Ni wazi Mkuu wa Mkoa wa aina ya Paul Makonda hawezi kufahamu mambo
makubwa kama haya. Kwake yeye na kwa Wakuu wa Mikoa au Wilaya wa aina
yake, kuwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa ni sawa na kuwa Rais wa Mkoa au Wilaya
aliyokabidhiwa.
Wakuu wa aina hii wanahitaji kuelimishwa kwamba wao hawana mamlaka ya kifalme aliyo nayo Magufuli.
Na namna bora kabisa ya kuwaelimisha ni kuwashtaki kwa madai mahakamani
pale wanapoenda nje ya masharti ya madaraka yao. Tutaanza na Paul
Makonda.

Tags
SIASA