Kufuatia Dar es Salaam kufanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne
kwa mwaka 2016 kwa kuingiza shule 6 kati ya kumi zilizofanya vibaya,
ofisi ya Elimu Mkoa imewaagiza wakuu wa shule na wakurugenzi kutoa
taarifa za kina juu ya sababu zilizopelekea kufanya vibaya.
Akiongea na TBC, kaimu Afisa elimu mkoa, Janeth Nsunza, alisema bado
wanaendelea na kikao kujadili tathmini ya matokeo hayo na wamesema
watatoa taarifa kamili watakapomaliza majadiliano.
Alisema, “Kati ya shule 10 ambazo hazikufanya vizuri shule hizo ni
Kitonga, Nyeburu, Mbopo, Mbondole, Somangila day na Kidete kufuatia
shule hizo sita kutofanya vizuri mkoa wa Dar es Salaam, mkoa umepokea
taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwani imekuwa ni kinyume cha
matarajio yetu na serikali yetu kwa ujumla.”
“Kwakuwa matokeo yametanganzwA, hatua za kufahamu nini hali hiyo
imejitokeza zimechukuliwa mara baada ya matokeo hayo kutangazwa ambapo
wahusika wanaendelea kutoa maelezo yao, licha kwa kuwepo kwa viashiria
katika mtihani wa Mock na wakurugenzi waliwaelekeza wakuu wa shule hizo
kuondoa hali hizo mapema,” aliongeza Nsunza.
Tags
ELIMU
