BANDA MEDIA BLOG

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWARA BORA ANJELAH LAIRUKI, AMEZINDUA OFISI YAKE ILIYOPO MJINI DODOMA, PROF KIKULA AWATOA WATANZANIA HOFU KUHUSU MUINGILIANO

WAZIRI wa nchi 0fisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala bora Anjelah Kairuki akiongea jambo kabla ya kuzindua rasmi ofisi yake mpya iliyopo Chuo kikuu cha Dodoma UDOM

Waziri huyo alikata utepe wakati alipokuwa akiizundua Ofisi hiyo Huku Makamu mkuu wa Chuo hicho Prof Idris Kikula, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt,Laurean Ndumbaro na Naibu Katibu Mkuu Susan Mlawi wakishudia
 Waziri Kairuki wakifurahia Jambo pamoja na Katibu mkuu wa Wizara hiyo wakati Waziri huyo alipomtembelea Ofisini kwa katibu huyo [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]








Waziri Kairuki, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt,Laurean Ndumbaro na Naibu Katibu Mkuu Susan Mlawi wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la ofisi za Utumishi lililopo UDOM

PICHA YA PAMOJA

Prof Kikula akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari kuhusu hisia kuwa kutakuwa na muingiliano chuoni hapo kati ya watumishi na wanafunzi

Na John Banda, Dodoma
WAZIRI wa nchi 0fisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala bora Anjelah Kairuki amezindua rasmi utoaji wa huduma kwa wananchi katika ofisi yake mpya iliiyopo chuo kikuu cha Dodoma Udom ambapo jumla ya watu 17 tayari wameshapatiwa huduma toka januari 30 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na watumishi wa wizara hiyo wakati wa zoezi la uzinduzi wa ofisi ya wizara hiyo Kairuki alisema kuwa ni sehemu ya kuunga mkono agizo la serikali kuhamia Dodoma.
Alisema kuwa ofisi hiyo ambayo ipo katika jengo la ofisi ya shule ya Sanaa na sayansi za jamii katika chuo kikuu cha Dodoma Udom na kuwataka wananchi wote wanaohitaji huduma yao kufika katika eneo hilo.
“Aidha napenda kutumia fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru wakala wa majengo TBA kwa kazi nzuri ya ukarabati na kuliweka jengo letu katika hali nzuri kwa kipindi cha muda mfupi ambapo inawawezesha watumishi kutoa huduma kama kawaida.
Aliongeza kuwa kutokana na uhamisho huo wa ofisi masula yanayohusu sera na sheria za utumishi wa umma na utawala wa utumishi wa umma ndiyo yatakayo tekelezwa katika ofisi ya Dodoma.
“Masuala ya usimamizi wa malipo ya mishahara, uendeshaji rasilimaliwatu, ukuzaji maadili, anuai za jamii, uchambuzi ushauri wa utendaji kazi na huduma ya teknolojia ya habari na mawasailiano kushughulikiwa na ofisi yetu ya Dar es saaalam kwa sasa kwa kuwa idara hizo zimepangwa kuhamia Dodoma katika awamu ya pili na tatu”alisema.
Naye makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma (Udom) Prof, Idris Kikula alisema kuwa jumla ya wizara sita zinatarajiwa kuweka makazi yake katika chuo hicho.
Kikula alisema kuwa haoni tatizo kwa serikali kuweka makazi yake hapo wakati wakiendelea kujipanga kutafuta eneo ambalo litakuwa ni la kudumu kwajili ya serikali tofauti na ambavyo watu wamekuwa wakisema katika mitandao ya kijamii.
“Watu wanadai eti muingiliano wa watumishi na serikali utaleta matukio ya vitendo vya umalaya lakini mimi kwangu naona huo ni mtazamo hasi ambao hauna tija mbona Ifm, Udsm, Cbe, Mipango kunamuingiliano wa watu na hakuna tabia hizo huwezi kuzuia munigiliano wa watu hata siku moja”alisema Kikula.
Hatahivyo alizitaja wizara hizo ambazo zinatarajiwa kuweka ofisi zake katika chuo hicho kuwa ni Katiba na sheria, Utumishi wa umma, Viwanda na Biashara, Afya, Elimu pamoja na Wizara ya mambo ya ndani ya nchi.
Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG