Staa huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwenye orodha ya mastaa
wanaotuhumiwa kubwia unga na walioamriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kujisalimisha kituo cha polisi central jijini Dar,
Ijumaa hii kwa mahojiano zaidi.
“Mimi kama Wema nimekuwa nikisemwa sana kuhusu kujihusisha na utumiaji
wa madawa ya kulevya na hata kujihusisha katika kuuza madawa ya
kulevya,” amesema Wema kupitia app yake.
“Sometimes wanasema nimefungwa, sometimes nimenyongwa, sometimes
nimekamatwa hususan pindi ninaposafiri kwenda nchi mbalimbali, na sasa
hivi nimeambiwa kwamba natumia madawa ya kulevya. Well, ni habari ambazo
mheshimiwa mkuu wa mkoa amesema hana uthibitisho nazo lakini amelazimu
kutaja majina kadha wa kadha ambayo ndio hivyo ameyataja mengine kwenye
vyombo vya habari, na ameamuru twende tukaripoti kesho (leo Feb 3),
ifikapo saa tano asubuhi,” ameongeza.
“Mi nasema hivi, nitaenda, nitaripoti, kwasababu ni wito ambao ametaja
mkuu wa mkoa wangu kuona amefanya, unaambiwa kubali wito, usikatae neno.
Kwahiyo tutaenda kesho, na ntamsikiliza yale ambayo anataka kuniambia,
iwapo tukishajua which is true, which is not, then tutajua from there
what to do, sasa hivi sina cha kusema, sina cha kufanya, because bado
sijaonana naye, kwa sasa niacheni tu nirelat but I want to assure you
one thing, I am not a drug addict, and I am not a drug abuser, and if I
was nadhani we all know how drug addicts act, we all know how drug
abusers wanakuwaga. I want you guys to relax, do not worry, everything
is going to be fine.”
Mastaa wengine waliotajwa ni TID, Mr Blue, Chidi Benz, Recho na wengine.
Tags
BIASHARA HARAMU
