Mwimbaji mashuhuri duniani na hasa katika bara la Afrika, Yvonne Chaka
Chaka amesema anatamani sana katika maisha yake kukutana na Rais
Magufuli.
Mwimbaji huo amesema Rais Magufuli anaugusa moyo wake kutokana na
utendaji kazi wake na ameshauri marais wengine wajifunze kutoka kwake
kutokana na utendaji kazi wake.
Amemalizia kwa kumpongeza Mama Salma Kikwete kwa kazi nzuri anazozifanya
katika kusaidia watoto hasa wasichana katika kupata elimu.
Tags
KIBURUDANI
