Rais
wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA, Ndibalema
John Mayanja (katikati), akizungumza Jijini Mwanza kwenye mkutano na
wadau mbalimbali wa biashara. Kulia ni Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani
Mwanza, Leopord Lema, na kushoto ni Mshauri TCCIA mkoani Mwanza, Lazaro
Kiheya.
BMG
Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA, Ndibalema Mayanja, amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa ya ununuaji wa hisa za kampuni ya TCCI Investment.
Mayanja ameyasema hayo Jijini Mwanza hii leo na kubainisha kwamba hisa hizo zilianza kuuzwa tangu Februari Mosi mwaka huu kwa bei ya shilingi Mia Nne na kwamba mwisho wa uuzwaji wa hisa hizo ni Machi 14 mwaka huu.
“Njia pekee ya kijiendeleza
kiuchumi hivi sasa ni kupitia hisa hivyo nunueni hisa hizi za kampuni ya
uhakika ambayo kila mwaka huwapatia wanahisa wake gawiwo lao”.
Amesisitiza Mayanja na kuongeza kwamba hisa hizo zinauzwa katika benki
ya CRDB na kwa mawakala mbalimbali walioidhinishwa na Mamlaka ya Masoko
na Dhamana (CMSA).
Mwenyekiti
wa TCCIA mkoani Mwanza, Joseph Kahungwa, amebainisha kwamba walionunua
hisa za TCCIA Investment mwaka 2005 kwa shilingi 250, hisa zao zimepanda
bei hadi shilingi 5,000 hivyo pesa hiyo iligawanywa na kupatikana bei
ya shilingi 400 ya kuuza hisa mwaka huu ambapo kwenye mauzo hayo kila
mwanahisa atapata gawio la hisa 12.5 kwa kila hisa moja.
Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leopord Lema, mesema
jumla ya hisa Milioni 112 zinatarajiwa kuuzwa lengo ikiwa ni kampuni ya
TCCIA Investment kupanua mtaji wake na kufikia Bilioni 45 kutoka
Bilioni Nane za mwaka huu 2017 ambazo zimeongezeka kutoka hisa Bilioni
Moja mwaka 2005 wakati kampuni hiyo inaanzishwa.Amedokeza kwamba hatua hiyo itasaidia TCCIA kuongeza uwekezaji wake ikiwemo ujenzi wa majengo ya kisasa na maghara ya kuhifadhia mazao katika mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Mtwara na Tanga pamoja na kuanzisha taasisi ya mikopo.
Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leopord Lema, akisisitiza juu ya umuhimu wa watanzanua kununua hisa za Kampuni ya TCCIA Investment. Pia amesema TCCIA itaendelea kushirikiana na serikali katika kuondoa changamoto za kiuwekezaji zilizopo ikiwemo upimaji wa maeneo ya ujenzi wa viwanda pamoja na uwanja wa maonesho ikiwemo Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki
Mshauri TCCIA mkoani Mwanza, Lazaro Kiheya akitoa neno la shukurani kabla ya mkutano huo kuahilishwa. Kulia ni Rais wa TCCIA, Ndibalema Mayanja.
Ameelezea umuhimu wa kila mfanyabiashara kuwa namba ya utambulisho wa biashara (TIN Number) na kuwasihi kutoa ushirikiano kwenye zoezi la uhakiki wa namba hizo ambapo amesema baada ya kufanyika Jijini Dar es salaam, litaendeleo Jijini Mwanza na maeneo mengine pia.
Picha ya pamoja.
Tags
UCHUMI / BIASHARA