Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Gabo Zigamba amewataka waongozaji
filamu Tanzania (Directors) kutojihusisha na kazi za kuongoza filamu
kama hawana vipaji pamoja na taaluma hiyo.
Gabo amesema watu hao ndiyo wanasababisha soko la filamu nchini kupigwa
bao na kazi kutoka nje kwa maana kazi wanazozitengeneza kukosa ubunifu
na ushindani kama ilivyokuwa zamani kupelekea watazamaji kuichukia
'Bongo Movie'.
"Kuwa 'director' siyo suala la kukurupuka tu, si maamuzi ya kufikirika
tu ukaamua kufanya hivyo lakini kila kinachofanyika lazima kiwe kina
taaluma ila nasisitiza na kuwaambia watu wasifanye vitu bila ya kuwa na
taaluma navyo, ukifanya kitu chenye taaluma nacho itakuwa kwenye
ubora".Alisema Gabo
Aidha msanii huyo amesema kwa upande wake watu wasahau kwa sasa kwa yeye
kuwa muongozaji filamu na kama atataka kufanya hivyo basi atafanya kwa
utaalamu na siyo kukurupuka.
