Baada ya kupewa muda kuwasalimia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa
Mjini Lindi, Ilulu leo tarehe 3 Machi 2017; Pamoja na mambo mengine Mama
Salma Kikwete amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge.
Kwamba, tukio alilofanya Rais tarehe 1 Machi 2017 kwa kumteua kuwa
mbunge limempa heshima kwake na mkoa wa Lindi kwa ujumla.
Tags
SIASA
