MSHAMBULIAJI wa Simba, Laudit Mavugo ameibuka na kusema kuwa siri ya
mafanikio ya kufumania nyavu hivi karibuni na kwenye mechi ya Yanga
kunatokana na bibi yake aliyekuwa Bujumbura, Burundi kumsapoti na
kumuombea kila siku.
Mavugo amekuwa na wakati mgumu wa kufumania nyavu tangu alipotua katika
kikosi hicho cha Msimbazi, lakini siku za hivi karibuni ameonekana
kuamka upya. Katika mchezo wa wikiendi iliyopita kati ya Yanga na Simba,
Mavugo alifanikiwa kufunga bao lake la saba kwenye Ligi Kuu Bara msimu
huu wakati alipoiongoza Simba kupata ushindi wa mabao 2-1.
Akizungumza , Mavugo alisema amekuwa katika wakati mgumu wa kuweza
kufunga lakini bibi yake aliyekuwa Burundi amekuwa akimuombea kwa muda
mrefu hasa katika mechi ya Simba na Yanga ili aweze kufunga hivyo bao
alilofunga anamzawadia yeye.
“Nimefurahi sana kuona nimefanikiwa kufunga, bao langu dhidi ya Yanga
namzawadia bibi yangu aliyeko Bujumbura kwani amekuwa akiniombea
nifunge hasa katika mechi hii dhidi ya Yanga.
“Mechi yetu na Yanga ilikuwa ngumu kwani kila upande ulikuwa ukihitaji
kuibuka na ushindi, nakumbuka kabla ya mchezo bibi aliniambia ananiombea
nifunge, hivyo bao hili yeye amehusika kwa kiasi kikubwa,” alisema
Mavugo.
Tags
MICHEZO KITAIFA
