Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) leo limemvua,
Maalim Seif nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Chama hicho na nafasi hiyo
kukaimiwa Bi. Magdalena Hamis Sakaya.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa CUF
Taifa, anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim
Lipumba amesema kuwa Baraza hilo limefiki uamuzi huo kutokana na sababu
mbalimbali ambapo moja wapo ni Maalim Seif kutofika ofisini na
kutohudhuria kwenye vikao vya chama vinavyotambulia kwa mujibu wa katiba
ya chama hicho.
“Miongoni mwa ajenda tulizo zijadili ni kuthibitisha wakurugenzi na
manaibu wakurugenzi, kupitisha jina la wagombea Ubunge wa Bunge la
Jumuiya ya Afrika Mashariki, kujaza nafasi za wajumbe wa Baraza Kuu
zilizokuwa wazi, kuunda Bodi ya wadhamini, kuunda kamati ya maadili,
taarifa ya fedha, taarifa ya kesi na taarifa ya hali ya kisiasa,”.
Pia Prof. Lipumba ametangaza majina matatu ya Wagombea Ubunge Bunge la
Afrika Mashariki kupitia majina yaliyoteuliwa na kikao cha Baraza Kuu la
Uongozi la Taifa kilichokaa Machi 25 na 26 mwaka huu.
Majina matatu yaliyoteuliwa na Baraza kuu la uongozi la Uongozi ni,
Sonia Magogo, Mohammed Habib Mnyaa na Thomas Malima mmoja kati yao
akitoa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mbali na hayo, Lipumba amemtangaza rasmi Bw. Abdul Kambaya kuwa
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma ambapo hapo awali
alikuwa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma.
