BANDA MEDIA BLOG

JAFFO AZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUCHAPA KAZI KWA BIDII


Mkuu
wa wilaya ya Longido mkoa wa Arusha,Godfrey Chongolo akizungumza wakati
wa zira ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)anayesikiliza kwa
makini na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halamshauri ya Longido,Juma
Mhina.

Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa
Chama cha Walimu mkoa wa Arusha,Lootha Laizer

Baadhi ya Madiwani na watumishi wa halmashauri ya Longido wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo

Baadhi ya Madiwani na watumishi wa halmashauri ya Longido wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo

Naibu
Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)akizungumza jambo alipotembelea
eneo linapojengwa soko la kisasa la mifugo katika Kijiji cha Orendeke
Kata ya Namanga mkoa wa Arusha,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Longido,Godfrey Chongolo.

Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo akizungumza na wananchi wa Kata ya
Makuyuni wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha baada ya kukagua ujenzi wa
Kituo cha Afya,serikali imetenga kiasi cha Sh 700 milioni kwaajili ya
upanuzi wa Kituo cha Afya Mto wa Mbu.

Muuguzi
katika Kituo cha Afya cha Usa River,Emiliana Sulle(kushoto) na Mganga
Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Bonifas Ukio(kulia)Mh.Suleiman Jaffo kumpima uzito mtoto ili kujua maendeleo yake.

Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)akiagana na Mbunge wa jimbo la
Monduli,Julius Kalanga baada ya kumaliza ziara yake mkoani Arusha.
   
Mwandishi wetu,Arusha
 
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo amewataka watumishi katika halmashauri
zote nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wawe wabunifu
katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
 
Katika ziara yake mkoani Arusha katika
halmashauri za Meru,Longido na Monduli alisema serikali imeshatoa fedha
za Mfuko wa Pamoja wa Afya(Basket Fund)katika halmashauri hizo hivyo
kukosekana kwa madawa na vifaa tiba sio jambo linaloweza kuvumilika.
 
Alisema miradi yote ambayo fedha
zimeshaletwa na serikali kuu kwenye halmashauri itekelezwe mara moja ili
iweze kuwahudumia wananchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG