Hapa
ni ndani ya ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga ambapo usiku wa Ijumaa Machi
3,2017 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanya sherehe ya kuuaga
mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 pamoja na kuwaaga wastaafu wa
jeshi la polisi.
Mgeni
rasmi katika sherehe hizo ambazo zimehudhuriwa na maafisa wa
polisi,wakaguzi,askari wa vyeo mbalimbali na wadau wa usalama alikuwa
mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack.
Akizungumza
wakati wa sherehe hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro
Jumanne Muliro alisema Machi 3 kila mwaka huwa ni siku ya Polisi ‘Police
Family Day’ ambapo pamoja na kuadhimisha siku hiyo,jeshi la polisi mkoa
wa Shinyanga limeamua kuwafanyia sherehe ya kuwaaga wastaafu 10 wa
jeshi hilo sambamba na kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.
“Tumeanza
sherehe hizi kwa mkuu wa mkoa kukagua gwaride katika uwanja wa Shycom
lakini pia kutoa tuzo kwa askari na wadau waliofanya kazi vyema mwaka
2016 katika ulinzi na usalama wa mkoa wa Shinyanga”,alisema kamanda
Muliro.
Naye
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack alitumia fursa hiyo
kulipongeza jeshi la polisi mkoani humo kwa kuendelea kuimarisha hali ya
ulinzi na usalama na sasa vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu wenye
ualbino yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Mwandishi wetu,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa sherehe hizo ametusogezea picha 65 za matukio yaliyojiri ukumbini
Ijumaa
Machi 3,2016 katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga-Aliyesimama ni
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
akizungumza wakati wa kufungua sherehe ya kuwaaga wastaafu wa jeshi la
polisi na kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.Kulia ni mgeni
rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.Kushoto ni mke wa kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga Mama Muliro
Kamanda
Muliro akizungumza wakati wa sherehe hiyo.Wa kwanza kulia ni Wakili wa
serikali mkuu mfawidhi Shinyanga Pendo Makondo akifuatiwa na jaji
mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela
Kamanda Muliro akizungumza ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza ukumbini.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwaomba wadau wote wa ulinzi na
usalama kuungana na jeshi la polisi kuendelea kushirikiana na jeshi la
polisi katika kuimarisha amani ya mkoa wa Shinyanga
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wastaafu wakiwa ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza ukumbini
Askofu
Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT),Dayosisi ya
Shinyanga, Dkt. John Nkola akiwasalimia wageni mbalimbali
Viongozi wa migodi na benki mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini
Wadau wa ulinzi na usalama wakiwa ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Wastaafu wa jeshi la polisi wakiwa wamekaa ukumbini
Kamanda
wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akiwasalimia wadau
walioshiriki sherehe hizo.Kushoto ni Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga
Annamaria Yondani
Askari wa jeshi la polisi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Wafungua Shampen wakijiandaa kufungua shampen
Zoezi la kufungua shampen likiendelea
Waandishi wa habari Moshi Ndugulile kutoka Radio Faraja na Frank Mshana wa ITV/Radio One wakiwa ukumbini
Viongozi wa dini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa sherehe
Wadau wakiwa ukumbini
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakigonga cheers na meza kuu
Zoezi la kugonga cheers likiendelea
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro (wa pili kushoto) akifurahia wakati wa kugonga cheers
Askofu
Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT),Dayosisi ya
Shinyanga, Dkt. John Nkola akigonga cheers na meza kuu
Zoezi la kugonga cheers
Wadau wakiwa katika foleni kwenda meza kuu kugonga cheeers
Mwenyekiti
wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kadama Malunde
akigonga cheers na mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro
Jumanne Muliro
Wadau wakiwa ukumbini
Sherehe inaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Sherehe inaendelea
Mke
wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
akifungua keki iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe ya kuwaaga wastaafu wa
jeshi la polisi.Katikati ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP
Muliro Jumanne Muliro.Kushoto ni MC Mama Sabuni
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwa ameshikilia
kisu kabla ya kukata keki.Wa pili kutoka kulia ni mwenyekiti wa kamati
ya maandalizi ya sherehe hiyo Elias Mwita
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro na mke wake
wakijiandaa kukata keki.Wa pili kutoka kulia ni mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya sherehe hiyo Elias Mwita
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akitabasamu kabla
ya kuanza kuwalisha keki wastaafu wa jeshi la polisi
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiendelea na zoezi la kuwalisha keki wastaafu wa jeshi la polisi
Tunafuatilia kinachoendelea……
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwalisha kesi
askari polisi na wadau waliofanya vizuri mwaka 2016 katika kuimarisha
ulinzi na usalama mkoani Shinyanga
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akimlisha keki mke wake
Mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akila keki
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya
Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela(katikati) na Wakili wa
serikali mkuu mfawidhi Shinyanga Pendo Makondo (kulia) wakifurahia jambo
ukumbini wakati kamanda Muliro akimlisha keki mke wake
Mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akikabishi keki kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kwa ajili ya meza kuu
Wadau wakiwa ukumbini
Sherehe inaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wastaafu wa jeshi la polisi
Zoezi la kukabidhi zawadi kwa wastaafu wa jeshi la polisi linaendelea
Zawadi zikiendelea kutolewa
Mstaafu akishikana mkono na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack
Wadau wakiwa ukumbini
Sherehe inaendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwapa zawadi wastaafu wa jeshi la polisi
Meza kuu wakiungana na mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuwapa zawadi wastaafu wa jeshi la polisi
Utoaji zawadi unaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Wadau wakitoa zawadi kwa wastaafu wa jeshi la polisi
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakipiga picha ya pamoja na mstaafu wa jeshi la polisi Anthony Gwandu (aliyekaa kulia)
Askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani wakifurahia ukumbini
Kamati ya maandalizi ya sherehe wakijitambulisha ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifungua muziki wakati wa sherehe
Ufunguzi wa muziki unaendelea
Wadau wakicheza muziki ukumbini
Meza kuu na wadau wakicheza muziki ukumbini
Muziki unaendelea
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Tags
HARUSI & SHEREHE