Mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo amewataka watu kuacha
kutumia lugha za maneno makali (matusi) dhidi ya wanawake kwa kuwa
wanawake ni watu wanaohifadhi maumivu na mambo mengi kwenye moyo zaidi
ya wanaume.
Jana wakati akikabidhi mchango wake EATV katika kampeni ya 'Namthamini',
Jokate amesema mwanamke ni mtu ambaye anakumbana na mambo makubwa
anayopaswa kukabiliana nayo mengine ni mazito lakini anayaweka moyoni
mwake ili kufanikisha jambo hivyo anapaswa kuheshimiwa.
"Najisikia vibaya sana pale ambapo mtu namsikia anatoa lugha ya matusi
kwa mwanamke, Wanawake tunaumia zaidi ya mara 1000 kwa mwanamke,
mwanamke anahifadhi mambo mengi sana moyoni kitu ambacho hakitakiwi,
wanawake wanapaswa kuheshimiwa na kulelewa katika jamii na wanastahili
kuthaminiwa". Amesema Jokate
Ameongeza kuwa yeye kwa upande wake mwanamke ni mtu mwenye moyo wa ziada
ambaye hujitoa kwa ajili ya jamii lakini pia ni mchapa kazi na anajua
kitu gani anataka.
Katika kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na EATV kuwachangia mabinti
waende shule bila kukosa kwa kigezo cha kuepuka aibu inayosababishwa na
ukosefu wa vifaa vya kujisitiri kipindi cha hedhi, Jokate amechangia
kiasi cha shilingi laki moja.
Tags
WANAWAKE
