Family bonding - muunganiko wa kifamilia ni jambo jema sana! Family
conflicts - migogoro ya kifamilia ni jambo baya sana... Msingi wa umoja
katika ukoo huanza kwenye familia
Tuna familia na koo zenye migogoro mingi sana vinyogo visasi wivu
dhuluma kijicho na mambo yanayofanana na hayo vimeharibu familia na koo
nyingi
Familia maarufu ya Gwajima ni mojawapo! Unapoona wanandugu wanatoa siri
za familia nje hasa kwenye vyombo vya habari kwa sababu yoyote ile jua
kuna shida kubwa ndani yake
Sakata la madawa ya kulevya limetuletea yatokanayo kwenye ukoo huu
maarufu wa Gwajima .....kwamba kaka yake Gwajima mchungaji aliugua hadi
kufariki na mdogo wake huyu akawaaminisha watoto wa marehemu kaka yake
kuwa angemfufua babayao (pengine kwa makubaliano fulani)
Kaka mtu hakufufuka ! Hakuna mtu aliyeyefufuliwa tena baada ya Yesu
Kristo kufufua aliowafufua. Watoto na ndugu wakajenga chuki na familia
ya Gwajima mchungaji na pengine hakuna waliohangaika kutatua huo mgogoro
kwa sababu wanaozijua wenyewe ama pengine walijaribu wakashindwa
Gwajima mchungaji ana kipaji na karama ya kuhubiri lakini anakitumia
vibaya. Gwajima ana uthubutu wa ajabu hayumbishwi na changamoto zake. Ni
watu wachache mno wenye hiki kipaji.. Kupitia hili amejijengea umaarufu
mkubwa na ni bilionea
Haya anayofanya ni laana kwa familia na ukoo wake, Gwajima ni muongo
sana lakini haogopi kuongopa ni mjanjamjanja mwenye viashiria vingi vya
utapeli kwa kutumia jina la Mungu na dini.... God is watching...!
Kutokana na hili haambiliki na amekuwa na kashfa na migogoro mingi
Kuna huyu Gwajima mwanasheria msomi asiye na tafakuri wala hekima! Kwa
kutaka kufurahisha kaliba Fulani ya watu na pengine kwa malipo kidogo
anamponda live kwenye media ndugu yake na kuleta ishu za kifamilia
upenuni... Zaidi pengine akiongozwa na wivu juu ya mafanikio ya nduguye
ambaye pengine hana elimu kama yake
Gwajima mchungaji hajaongea bado kumjibu lakini wawili hawa wanatupa mwanga wanajifunua wakoje huko kwenye ukoo wake
Kaka mbabe jeuri Mdogo mtu msomi asiye na hekima wala weledi kila mtu ana watu nyuma yake
Wameanza kumalizana live mpaka nje laana hii itadumu vizazi vingi
Tags
AAH
