Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 10 Machi, 2017
ameongoza Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino
Mkoani Dodoma.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wake wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa
CCM Zanzibar ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara
Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.
Tags
CCM
