Bado sakata la mama wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu , Mariam Sepetu
kudaiwa kumrekodi bila ridhaa yake mchekeshaji Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ kisha sauti hiyo kuitupia mitandaoni, kuna siri mpya imebainika
ndani yake ya kuwatimua wanaume tata ‘mashoga’ nyumbani kwa mwanaye
huyo.
Katika sauti hiyo ambayo, mama Wema alisikika akimshushia lawama nzito
Steve kwa kitendo chake cha kutokwenda kumuona Wema aliposhikiliwa
mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar ‘Sentro’ na Steve kujitetea
kwamba alifanya hivyo kwa sababu alikwenda Dodoma kuonana na wabunge ili
wamsaidie Wema kutoka, lakini jambo jipya ni mama Wema kukiri
kuwafukuza mashoga hao nyumbani kwa mwanae.
Mama Wema katika mazungumzo yake kwenye sauti hiyo, alisema kuwa yeye
hapatani au hafugi ujinga na ndiyo maana hata ‘wale’ mashoga waliokuwa
nyumbani kwa Wema, Ununio, aliwatimulia kwa mbali. “Mimi sipendagi
ujinga. Wale mashoga nimewafukuza wote pale, hawapo tena…” alisikika
mama Wema akimwambia Steve Nyerere huku akitumia sauti ya kujigamba.
Kumekuwa na madai kwamba, baadhi ya mastaa Bongo wamekuwa wakiishi na
wanaume ‘tata’ (mashoga) bila kujulikana madhumuni yake.
“Unaweza kukuta staa anaishi na mashoga watatu mpaka wanne na imekuwa
fasheni sasa, kila staa anao nyumbani kwao, sijui kwa madhumuni gani?”
kilihoji chanzo kimoja baada ya kumsikia mama Wema akidai kuwatimua
mashoga hao nyumbani kwa binti yake. “Kwa sauti hii, nimeamua mama Wema
si wa mchezomchezo.
Unajua mama kufunga safari mpaka nyumbani kwa binti yake na kutibua utaratibu wake si jambo dogo.
“Wa mama wengine wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu wanaamini binti au
mtoto kwa vile ameshafikisha miaka 18 basi ni mkubwa anatakiwa
kujitawala. Noo! Mtoto ni mtoto tu, kwa mama hakui hata angekuwa
mkubwa,” kilizidi kusema chanzo hicho.
Miezi ya nyuma, msanii wa filamu aliyewahi pia kuwa mtangazaji, Lulu
Semagongo ‘Aunty Lulu’ aliwahi kuandikwa kwa habari za kudaiwa kuishi na
mashoga. Lakini pia baadhi ya mastaa wamewahi kuandikwa kwa madai ya
kuwa karibu sana na
Tags
SIASA
