Kwa upande wake Gwajima, juzi alitumia ibada kwenye kanisa lake lililopo
Ubungo-Maji kuonesha cheti cha matokeo ya kidato cha nne alichodai ni
cha Makonda kilichoonesha alipata alama F kwenye masomo yote alipohitimu
katika Shule ya Sekondari ya Pamba jijini Mwanza.
Gwajima alisema ngoma bado mbichi baada ya video iliyoenea mtandaoni
ikionesha Makonda akivamia kwenye Ofisi za Clouds kwa kile kinachodaiwa
kushindwa kurushwa hewani mahojiano ya mwanamke anayedaiwa kuzaa naye.
“Anachokifanya ni kuwasha moto wakati hana Zima Moto, kama Daudi Bashite
ataendelea kunichokonoa, nitakuja na makombora mengine, nitapiga na
moshi utatoka,” alisema Gwajima.
Tags
Askofu Gwajima
