Rais wa 45 wa Marekan,Donald J Trump ni moja ya binadamu wenye mafanikio
sana duniani, japo kisiasa watu wanaweza kumbeza lakini huyu ni mtu
ambaye anajua maana ya mafanikio, wakati wa mahojiano yake kipindi ana
anza kugombea urais alisema 'i always win, i am a winner" maisha yake
japo yamekuwa na kupanda na kushuka yana rekodi mbali mbali, zifuatazo
ni baadhi tu ya rekodi za Maisha ya bwana Trump.
Trump; mafanikio kama mfanyabishara na raia wa kawaida
1. Trump yuko kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha guinness, kwa kuwa
mfanya biashara aliye wahi kufanya "biggest financial turnaround in
history" , kwani Alikuwa bilionea aka filisika na kuwa na madeni yanayo
fikia dola za marekani Bilioni moja, ali jikwamua na kurudi kuwa
bilionea tena. Ni rekodi ya dunia hiyo
2. Trump pia yuko kwenye kitabu cha guiness kwa kuweza kufanya dili ya
haraka ya zaidi iliyo husisha mamilioni ya dola, ambapo ali present plan
zake kwa dakika tatu na wakakubaliana na bwana Ricardo Ballino kufanya
dili hiyo ya pesa nyingi.
3. Donald Trump ni binadamu aliye fanikiwa kutoa hotuba na kulipwa pesa
nyingi kwa saa, kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa akichaji dola za
marekani milioni 1.5 kwa lisaa. Alikuwa akitoa semina za real estate
expose.
3.Donald Trump, ni mmoja kati ya wamarekani 256 tu ambao ni mabilionea.
4. Dolad Trump, amefanikiwa ku pata heshima na tuzo mbali mbali kama
mwana burudani, kama vile Hollywood walk of fame, kwa mchango kwenye
burudani, na WWE hall of fame kwa mchango wake kwenye mchezo wa mieleka.
5. Ni mwandishi mbali mbali wa vitabu ambavo viliuza zaidi, kitabu
maarufu kikiwa Art of the deal ambacho kiliuza zaid miaka ya 80, pia ni
moja ya vitabu vitano vya juu kuuza zadi kwa kufikisha nakala milioni
moja zilizo uzwa, kwa kizungu tuna seme best seller.
6. Donald Trump, amewahi kuongoza kipindi cha burudani namba moja kwa
Amerika, ambacho ni the apprentice, kwa wale mnao kumbuka miaka ya 2005
tumeangalia sana hiko.
Trump;Rekodi za Siasa
1. Rais Tajiri kuliko wotee waliopata kuwepo marekani ana kadiriwa kuwa na utajiri wa usd bilioni3-5
2.Rais aliye shika madaraka akiwa na umri mkubwaa kuliko wote kwenye historia ya USA, alikuwa na miaka 70.
3.Rais pekee wa Marekani ambaye hakuwahi kuwa mwanasiasa au kiongozi mkubwa wa jeshi, haija wahi tokea hii.
4. Rais pekee ambaye amewahi kuoa zaid ya mara 2. Wenzetu hujali sana
familly value talaka zikizid huwa ni ngum kuchaguliwa ila jamaa
alipenya.
5.Trump ni mgombea pekee ambaye anadhaniwa alishindwa midahalo yote mitatu na akafanikiwa kushinda urais
6. Trump ni mgombea pekee katika miaka 40 kutoweka wazi malipo yake ya kodi na kushinda uraisi.
7.Trump ni mgombea pekee ambaye, pamoja na kuchukiwa kuliko wagombea
wote kwenye historia ya marekani, bado alishinda uraisi(Alikuwa ana
kubalika kwa asilimia 32 tu)
8.Trump ni mgombea pekee ambaye alipoteza kura za jumla karibu milioni 3 na bado alifanikiwa ku ukwaa urais wa Marekani.
9.pamoja na kupingwa na Rais, makamu wake, first lady, speaker ,
mawaziri, maseneta na viongozi wa chama chake woote, ni watu wa wili tu
wa marekani waliowahi kufanikiwa kushinda vikwazo kama hivo na kuwa
marais wa Marekani, Andrew Jackson 1828,na Donald Trump 2016.
Umpende au usimpende lazima tukubali kuwa Rais Trump ni moja ya binadamu ambao wamefanikiwa kwenye maisha yao.
Tags
Donald Trump
