Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema
suala la uvamizi wa kituo cha Clouds Tv wahusika wanatakiwa kuripoti
tukio hilo Polisi haraka.Amesema atafuatilia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kinondoni, Suzan Kaganda kama tayari limeripotiwa kwa hatua zaidi