WAZIRI Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward
Lowassa, amemwomba Rais Dk. John Magufuli kufuta kauli yake ya kuwazuia
wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kushirikiana na wabunge wa
upinzani.
Akizungumza jana katika ziara viongozi wa Chadema katika mikoa ya Pwani
na Dar es Salaam, Lowassa alisema kauli hiyo Rais Dk. Magufuli inabomoa
misingi ya amani iliyojengwa na waasisi wa taifa letu.
'”Namuomba Rais (Magufuli) aondoe kauli ile aisahihishekauli hiyo na
nawaomba watanzaniatukatae kugawanywa…tusikubali nchi hii ni yetu sote
hakuna mtu mwenye haki miliki hapa ikienda vibaya tunaangamia wote
ikienda vizuri tunafaidi wote kwahiyo tukatae,” alisema
Alisema Watanzania wamekuwa wakiishi bila ya kubaguana kwa misingi ya
dini, rangi au ukabila na kukumbushia kauli iliyowahi kutolewa na baba
wa taifa kuwa ubaguzi ni sawa sawa na kula nyama ya mtu, ukishakula
hutotaka kuiacha.
Mjumbe wa huyo wa Kamati Kuu alisema hali ya maisha imezidi kuwa ngumu, huku bei ya bidhaa ikizidi kupanda kila siku.
Kutokana na hali hiyo alisema CCM kiliiba sera ya Chadema, ikiwemo elimu bure, lakini imeshindwa kuitekeleza.
“'waliiba sera na ilani yetu ya uchaguzi, lakini kwa kuwa hawakujiandaa wamefanya hali kuwa ngumu sana,” alisema
Katika kikao hicho cha ndani cha kuimarisha chama, Lowassa ameeleza
tatizo la ajira linavyozidi kuwa kubwa na kuongeza kuwa mipango mibovu
imesababisha sekta binafsi kuyumba, huku makampuni kadhaa na shughuili
nyingine za kutoa ajira zikifungwa na kusababisha ongezeko kubwa la
wasiyo na ajira.
Kuhusu ushirikiano miongoni mwa vyama vya upinzani, Lowassa alisema
Ukawa ni muhimu kuliko wanavyoweza kudhani kwani muunganiko wa vyama vya
siasa katika karne hii ni jambo la muhimu.
“Kikubwa cha kuzingatia ni umoja na mshikamano. Watanzania wana imani
kubwa sana na chadema kwa sasa na kama kuna mtu anatafuta chama mbadala
cha kuhamia basi ni Chadema,” alisema
Tags
Edward Lowassa
