Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Felix Kaweesi amepigwa risasi
na kuuawa na watu wasiojulikana. Taarifa zinasema Bw Kaweesi ameuawa
baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa
anaondoka kwake nyumbani Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji
mkuu Kampala.
Walinzi wake wawili walioandamana naye pia wameuawa.
Bw Kaweesi aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana.
Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo
kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake.
Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.
Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mulago.
Tags
Uganda
