Watu kumi na tano wamekamatwa na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es
Salamu kwa kosa la kukaidi agizo la serikali lililowataka kuondoka
maeneo ya mabondeni.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Saimon Sirro amesema
watu hao wamekamatwa na kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukaidi
kuhama maeneo hatarishi na kwamba eneo hilo ni mali ya halmashauri ya
manispaa ya Ilala.
Hata hivyo kamanda Sirro amesema hali ya usalama katika jiji la Dar es
Salaam imetengamaa, ambapo jeshi hilo limefanikiwa kudhibiti vikundi vya
kihalifu.
Aidha jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata wezi wa magari na uchunguzi bado unaendelea.
Tags
KOLOKOLONI
