Akihojiwa Jana, Msukuma alidai kwa walichokifanya watu wanaodaiwa ni
askari kumuonyesha bastola mhe Nape ni sahihi kwani kitambulisho cha
askari yeyote ni bastola au bunduki hivyo Nape hakupaswa kuwa na shaka
maana walikuwa wanamlinda. Msukuma alienda mbali zaidi na kusema hata
yeye alionyeshwa SMG nane lakini hakuwa na shaka maana wale ni askari.
Aidha Msukuma Alisema Kuwa Mhe Nape Alipaswa Kutulia kwanza hata kwa miezi mitatau ndipo angezungumza aliyotaka kuzungumza.
Pia Amemsihi Mhe Nape Kuacha Hasira mara baada ya kutenguliwa kuwa
Waziri kwani wakati anaomba kura katika jimbo lake la Mtama aliomba
hakuomba na uwaziri ,hivyo asilie kuenguliwa katika wazifa huo kwani
bunge lina wabunge 360 na kila mbunge angependa kuwa waziri,hivyo
kuenguliwa kwake katika nafasi hiyo inawapa nafasi wabunge wengine nao
kuwa mawaziri siku moja na hata yeye anatamani kuwa waziri
