Mtandao
wa Jinsia (Tanzania Gender Network Programme- TGNP) umetoa mafunzo kwa
waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga nakwa ajili kuwajengea uwezo
kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa
muda wa siku mbili (Machi 2 na Machi 3 mwaka 2017 katika ukumbi wa
Vijana Center katika kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini
Shinyanga pia yamewakutanisha waandishi hao wa habari na viongozi wa
vituo vya taarifa na maarifa vilivyopo wilayani Kishapu mkoani
Shinyanga.
Akizungumza wakati wa mafunzo
hayo,Mratibu wa mafunzo hayo ambaye pia ni mwezeshaji Bi Nyanjura
Kalindo alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea uwezo waandishi wa
habari kuhusu masuala ya kijinsia na kuwakutanisha na wanaharakati wa
masuala ya kijinsia kutoka kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ili
kuongeza nguvu ya pamoja.
“Vipaumbele vya TGNP ni vitano
ambavyo ni afya,elimu,kilimo,uziduzi na maji hivyo kwa kuwapatia mafunzo
waandishi wa habari tunaamini kabisa itaongeza chachu kuandika habari
kwa usahihi zaidi kuhusu masuala ya kijinsia”,alieleza Kalindo.
Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo
Bwana Rasel Madaha aliwaomba waandishi wa habari kufika katika maeneo ya
pembezoni kwani vitendo vya ukatili wa kijinsia yapo na hayaandikwi
hali inayosababisha vitendo hivyo kuendelea kujitokeza na kuwafanya
baadhi ya watu kuendelea kunyanyasika.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo
Nyanjura Kalindo akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari
mkoa wa Shinyanga iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya kijinsia
Mwandishi wa habari gazeti la
Nipashe Marco Maduhu akichangia mada wakati wa semina/mafunzo hayo.Kulia
kwake ni wanaharakati wa kupinga ukatili wa kijinsia kutoka kata ya
Mwadui-Luhumbo wilayani Kishapu wakiwa ukumbini
Mwezeshaji Nyanjura Kalindo kutoka mtandao wa jinsia Tanzania akitoa mada ukumbini
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Rasel Madaha akizungumza ukumbini
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Rasel
Madaha akiwasisitiza waandishi wa habari kuandika habari zinazohusu
watu wasio na sauti katika jamii
Mwandishi wa habari wa radio
Free Africa Malaki Philipo (kulia) na Steve Kanyefu kutoka Radio Faraja
fm stereo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na mwezeshaji Rasel
Madaha
Mwezeshaji Rasel Madaha akiendelea kutoa mada
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na mwezeshaji wa mafunzo hayo Rasel Madaha
Mafunzo yanaendelea.Kulia ni
mwanaharakati wa masuala ya jinsia kutoka wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga Kasigwa Adram,katikati ni mwandishi wa habari Sam Bahari
akifuatiwa na Charles Jilala ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya
kijinsia kutoka wilayani Kishapu
Katikati ni mwandishi wa habari
wa DW,Veronica Natalis akifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.Wa
kwanza kushoto ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Elizabeth Joseph
kutoka wilayani Kishapu
Mwandishi wa habari wa gazeti la
Jamboleo Stephen Kidoyayi akichangia mada ukumbini.Kushoto ni mwandishi
wa habari kutoka Radio Faraja,bi Moshi Ndugulile
Katikati ni mwanaharakati wa
masuala ya kijinsia Rahel Madundo akiwa na washiriki wa mafunzo hayo
wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Marco Maduhu akichangia mada wakati wa mafunzo hayo
Kushoto ni mwandishi wa habari
wa gazeti la Mwananchi Stella Ibengwe akifuatiwa na Kareny Masasy wa
gazeti la Habari leo na Wezay Ally kutoka radio Faraja
Mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja Steve Kanyefu akichangia mada ukumbini
Mwanaharakati wa masuala ya
kijinsia Rahel Lisesi kutoka wilayani Kishapu akielezea changamoto
zinazowakabili wananchi wanaozunguka mgodi wa madini ya almasi wa
Williamson uliopo Mwadui wilayani Kishapu
Mwandishi wa habari wa Azam
TV,bwana Stephen Wang’anyi akichangia mada ukumbini.Kulia kwake ni
mwandishi wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde
Mwandishi wa habari wa Malunde1 blog,Kadama Malunde akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru na Mzalendo,bwana Chibura Makorongo(aliyenyoosha mkono) akichangia hoja ukumbini
Kushoto ni mwezeshaji Nyanjura Kalindo akisisitiza jambo ukumbini
Mwandishi wa habari kutoka radio Faraja,Steve Kanyefu akichangia mada wakati wa mafunzo hayo
Kushoto ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia
Mwanaharakati wa masuala ya
kijinsia kutoka wilaya ya Kishapu Charles Jilala akizungumzia changamoto
mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata ya Mwadui-Luhumbo wilayani
humo katika sekta ya afya,elimu,kilimo,uziduaji na maji
Mwandishi wa habari kutoka radio Faraja Simeo Makoba akiwa amenyoosha mkono kwa ajili ya kuchangia mada
Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Rahel Madundo akielezea changamoto zinazowakabili wananchi wilayani Kishapu

Picha ya pamoja baada ya mafunzo
Picha ya pamoja
Picha
ya pamoja ,wawezashaji wa mafunzo hayo,Rasel Madaha (kushoto) na
Nyanjura Kalindo na Mwandishi wa habari wa Malunde1 blog,bwana Kadama
Malunde ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga (SPC)
Picha na Frank Mshana,Stephen Wang’anyi na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Tags
HABARI KITAIFA




