![]() |
| Kushoto: Mama Margaret Aswani & Kulia: First Lady wa Kenya Mama Margaret Kenyatta. |
Kwenye zile za watu kufananishwa na mastaa au watu wengine wakubwa na
maarufu duniani ongeza na hii ya huyu mama anayefananishwa na First Lady
wa Kenya, Mama Margaret Kenyatta.
Nimekutana na stori kwenye mtandao mmoja wa Kenya ya mama mmoja aitwaye
Margaret Aswani anaedaiwa kufanana sana na mke wa Rais wa Kenya, Mama
Margaret Kenyatta.
Kwa mujibu wa mtandao huo, Mama Aswani amekuwa akipewa msaada na
upendeleo fulani kwenye sehemu mbalimbali za umma kama vile Supermarket,
Benki, na sehemu nyingine kutokana na watu kumfananisha sana na First
Lady wa nchi hiyo Margaret Kenyatta.
Mwaka 2015 mama Aswani alihudhuria shererhe za Marathon za ‘Beyond Zero
Marathon’ na kuwachanganya Wakenya wengi waliostajabishwa na kufanana
kwa mama huyo na mke wa Rais wa nchi hiyo.
Je, wewe unaonaje, ni kweli mama Margaret Aswani kafanana na First Lady Mama Margaret Kenyatta? Niahcie comment yako hapa chini.
Tags
MAAJABU
