Abraham Lincoln...mmoja wa marais wa zamani wa USA alipata kusema
serikali bora ni ile ya watu, inayotokana na watu, kwaajili ya watu".
Katiba ya Jamhuri ya Muungano imesisitiza kuwa wananchi ndiyo msingi wa
madaraka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yote kutoka kwa
wananchi. Katika ulimwengu wa kidemokrasia, kushirikisha na kuheshimu
maoni ya wananchi ndiyo njia ya kwanza na ya msingi kabisa kwa serikali
kutimiza mamlaka ya mwisho waliyonayo wananchi.
Sasa huyu anayepuuza maoni, malalamiko na ushahidi wa wazi wa wananchi
dhidi ya Bashite, amepoteza sifa zote za uongozi zinazokubalika
duniani.
Baba wa Taifa, Nyerere, alipata kusema "madaraka hulevya, na madaraka zaidi hulevya zaidi"
Huyu anayesema hapangiwi, haonyweshi njia ya kupita, eti aliamua
mwenyewe kuwa Rais baada ya kujiona anafaa; huyu anayedhani kujiamini ni
kutosikiliza wananchi na kumlinda yule ampendaye yeye tu; sio Kiongozi
tena. Ni Mlevi wa Madaraka. Hii ni fursa nyingine kwa Watanzania
kutafakari na kuchukua hatua sahihi dhidi ya hatari inayotukabili ya
kuendelea kuongozwa na Mlevi
Pale uvunjaji wa sheria na ukosefu wa haki inapokuwa , jambo la kawaida
katika jamii yetu .hasa inapofanywa na viongozi wetu ,kuipinga hali na
tabia hiyo inapaswa kuwa wajibu wetu sote!
Peter Msigwa The MP
