Imebainika kuwa njama za kumtoa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul
Makonda zilianza Bungeni kwa kuratibiwa na baadhi ya wabunge
wanaohusishwa na mtandao wa dawa za kulevya.
Katika kudhibitisha hili, walifanya kikao Dodoma kilichohusisha baadhi
ya wabunge na kukubaliana kuunganisha nguvu na wafanyabiashara na
Viongozi wa Dini waliohusishwa na biashara ya Dawa za kulevya.
UTEKELEZAJI WAKE :-
1. Walikubaliana kuungana na baadhi ya viongozi wa ukawa ambao hapo
awali walikuwa mahasimu wao kisiasa, zoezi lililoratibiwa na mbunge
mmoja ambae ni mtoto wa kiongozi mstaafu, rejea picha za matukio
mbalimbali wakati wa mechi ya simba na yanga (zoezi lilifanikiwa)
2. Kuwaunganisha kwenye mtandao wafanyabiashara wakubwa waliotajwa na
Makonda pamoja na kumuunganisha Askofu mmoja alietuhumiwa kujihusisha na
mtandao wa dawa za kulevya, lengo la kuwaunganisha hawa ni kupata
ufadhili wa fedha za kutosha, rejea kauli za baba askofu akidhibitisha
kujizatiti kumuondoa Makonda Dar (zoezi lilikamilika)
3. Kushawishi marafiki wakubwa wa makonda ambao walikuwa wakimsaidia
Makonda katika vita ya dawa za kulevya kwa kuwarubuni kumgeuka makonda
na kuungana katika kambi yao kwa makubaliano kuwa makonda akiondoka Dar
watashinikiza kupatikana kwa mkuu wa mkoa ambae atakuwa hana purukushani
za dawa za kulevya, udhibitisho wa hili ni RUGE KUMGEUKA MAKONDA(zoezi
limefanikiwa)
4. Kutumia baadhi ya mawaziri ambao watu wao walijeruhiwa kwenye kampeni
za uchaguzi na kuwaingiza kwenye mtandao wa kumtoa Makonda Dar,
ushahidi wa hili ni alliance ya Mgombea wa Urais kutoka Lindi, mahusiano
yake na waziri ambae amejitoa Muhanga kumpinga Makonda hadharani.(zoezi
lilikamilika tangu dodoma)
5. Kutengeneza tukio ambalo litamfanya makonda apate aibu mjini, kisha
wamtake makonda aaibike, wakishapanga mtego mmoja makonda akaujuaga mida
ya nyuna akukwepa, sasa hili tatizo la makonda kwenda CLOUDS usiku
lilivyotokea wakaamua KUKANYAGIA HAPO HAPO.
6. Kuwashawishi baadhi ya wabunge wa chama tawala kutoa vitisho kama
Makonda hataondolewa kwenye ukuu wa mkoa basi watajiuzulu , ushahidi wa
hili ni post ya face book ya mhe Kingu(zoezi lilifanikiwa)
HITIMISHO
-Jiulize tangu lini clouds na mmiliki wa ipp walishakuwa na mahusiano ya karibu kama juz?
- Jiulize tangu lini EFM na CLOUDS walishakuwa marafiki?
- Jiulize tangu lini Askofu alishawai kukaa karibu na CLOUDS?
- Jiulize tukio linalotajwa la uvamizi limetokea ijumaa, kelele zimeanza
kupigwa Jumatatu hii ni baada ya hawa mabwana kukutana jumamosi na
kufanya kikao cha pamoja jumaosi na jumapili hela ikatoka kanisani kwa
askofu kwa kazi maalum Jumatatu.
-Jiulize hiyo jumatatu jamaa kafanya mahijiano live asubuhi, kisha saa
nne asubuhi Mhe waziri anatinga CLOUDS akiwa na mzee wa ipp, na hapo
hapo kamati ya huduma za bunge inakwenda CLOUDS mchana huo huo?
-Jiulize kwa nini wote wameshinikiza Makonda aondolewe Dar?
Na mwisho kabisa, baada ya Mhe Rais Dkt. John Magufuli kustukia njama
zao kutokana na kuwa na kikosi imara cha ujasusi katika maeneo
mbalimbali akawabomoa LIVE bila chenga pale ubungo wakati wa uzinduzi wa
mradi wa flyover.
TUKIDHANI WATAMUELEWA MHE RAIS WAMEGOMA NA KUMSHAWISHI MHE WAZIRI KUUNDA
KAMATI WAKATI WANAJUA MHE RAIS AKISHAONGEA MJADALA UMEKWISHA, LAKINI
WAO WAMEAMUA SASA KUPAMBANA NA NGUVU ZA MHE RAIS KWA KUSHINIKIZA BAADHI
YA WABUNGE WAJIONDOE KWENYE NYADHIFA ZAO.
NB:Hayo ni Maoni ya Mmoja wa Msomaji Wetu na Wla Si Msimamo wa Blog
Hii,Sisi Kazi Yetu ni Kufikisha Taarifa Tu,na Hata Wewe Unaweza
Kuwasiliana nasi kuweza Kuandika Makala ya Maoni Yako Hapa
Tags
Paul Makonda
