Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema taratibu
zitafuatwa kuwawajibisha viongozi wake na wa serikali wanaokabiliwa na
tuhuma na madai mbalimbali.
Polepole amesema hayo jana katika Makala ya Kinagaubaga, kipindi
kinachorushwa na Idhaa ya Kiswahili ya Deutschen Welle(DW) baada ya
kuulizwa swali kuhusu chama hicho kulea utovu wa nidhamu wa makada wake,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru, Alexander Mnyeti wanaotuhumiwa kulidhalilisha Bunge na chombo
hicho kwa kauli moja kutaka wajieleze.
Akijibu swali hilo Polepole alisema, "Ninyi hamkujua kama tutawachukulia
watu juzi, Serikali ina utaratibu wake bunge lina utaratibu wake na
chama kina utaratibu wake. Tunao utaratibu tunafuata, wananchi wawe na
subira"
"Wananchi wawe na subira, ninafahamu wananchi wana subira sana, wasubiri
mamlaka za viongozi, hawa wote waliokosea, mchakato wa haki ufanyike na
hatimaye tutaona matunda yake."
Tags
CCM
