Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari Mkoani
Dodoma kuhusiana na kufuta agizo lililotolewa jana na Waziri wa Katiba
na Sheria kuhusu Wananchi wanaohitaji kufunga ndoa kuanzia mwezi Mei
mwaka huu kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Rais Mhe. Dkt. Magufuli ameagiza
utaratibu wa awali uendelee kutumika kwasababu wananchi wengi wa
Tanzania hawana vyeti, hivyo wangekosa haki hiyo ya kufunga ndoa.
Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana. PICHA NA IKULU
Tags
SERIKALI