Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju leo amewasilisha Muswada wa
Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za mwaka 2017, unaokusudia kufanya
marekebisho katika baadhi ya sheria.
Akizungumza mbele ya Kamati hiyo Masaju alisema sheria zinazopendekezwa
kurekebishwa katika Muswada huo ni ya Bajeti, Sura ya 439 na Sheria ya
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura namba 264.
Alisema marekebisho hayo yanafanyika kwa lengo la kuondoa upungufu
uliojitokeza wakati wa kutumia sheria hizo pamoja na kuongeza masharti
mengine ili kuleta uwiano kati ya zinazorekebishwa na zilizopo.
Tags
SHERIA