STRAIKA wa Yanga Obrey Chirwa amesema bado wana nafasi ya kuchukua
ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa bado wataendelea kupambana
vizuri kwenye mechi zijazo ili kupata matokeo mazuri.
Chirwa ambae kwasasa amekuwa na msaada mkubwa katika kikosi cha Kocha
mkuu George Lwandamina, huku akiwa amepachika magoli nane katika ligi
kuu tangu alipo sajiliwa na Yanga akitokea Platinum ya Zimbabwe.
Chirwa amesema “Huwezi kututoa kwenye mbio za ubingwa kwa mechi mbili ambazo kwetu tumeambulia alama moja.
“Mimi bado naamini tukishikamana vizuri kuanzia viongozi hadi wachezaji
nina imani kombe linabaki mitaa ya Jagwani,” alisema Chirwa.
Nyota huyo ambae usajili wake ulizua gumzo kwa mashabiki hadi kwa
wazee wa Yanga kama (mzee Akilimali) huku wakimuona hafai amesema penati
aliyokosa Msuva ilisababishwa na uwanja kuwa mbovu.
Tags
MICHEZO KITAIFA
