Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Democrasia na Maendeleo
(Chadema) Kanda ya Pwani Mhe. Frederick Sumaye ameiomba serikali
kusimamia misingi ya demokrasia katika kutatua malalamiko ya wananchi na
kusimamia ustawi wa jamii ya Watanzania.
Mhe. Sumaye ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa
kama serikali itafanyia kazi malalamiko na mapendekezo yanayotolewa na
wananchi ni wazi taifa litafikia malengo yake iliyojiwekea ya kupunguza
hali ya umasikini na kuongeza pato la taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo Mhe. Sumaye amewaasa watendaji wa serikali kutumia vizuri
misaada inayotolewa na nchi wahisani ili kuhakikisha fedha za wananchi
zinazotumiwa katika ulipaji wa madeni hayo zinakuwa na manufaa kwa
watanzania wote hasa wale wasiofikiwa na huduma muhimu za kijamii.
Tags
Sumaye
