Mkurugenzi
wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akieleza kwa ufupi kuhusiana na
uzinduzi wa mashine za kutolea pesa za benki ya UBA ambapo Benki hio
imezindua mashine hizo za kutolea pesa katika vituo vinne kwa hapa Dar
Es Salaam
Mwenyekiti
wa Bodi ya Benki ya UBA Bank, Jenerali Mstaafu Robert Mboma akikata
utepe pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya UBA Tanzania Mh Peter Makau
kuashiria uzinduzi wa mashine za kutolea pesa katika vituo vinne ndani
ya jiji la Dar Es Salaam
Mwenyekiti
wa bodi ya Benki ya UBA Tanzania, Jenerali Mstaafu, Robert Mboma
akikata utepe mbele ya Mashine ya kutolea pesa ya benki hiyo mapema leo
katika uzinduzi wa vituo vya kutolea pesa vya benki hiyo.
Mkurugenzi
wa benki ya UBA Tanzania, Mh Peter Makau akitoa pesa katika mashine ya
kutolea pesa ya benki ya UBA Tanzania mara baada ya uzinduzi kufanyika
katika kituo cha Mikocheni. Mashine hiyo ya kutolea pesa ya UBA bank ipo
katika Kituo cha Mafuta cha Oilcom kilichopo Mbezi chini.
Mkurugenzi
wa benki ya UBA Tanzania, Mh Peter Makau akisubiria pesa katika mashine
ya kutolea pesa ya benki ya UBA Tanzania mara baada ya kuiamuru mashine
kutoa pesa mara baada ya uzinduzi wa mashine hizo uliofanyika leo
katika kituo cha Mafuta cha oilcom kilichopo mbezi chini
Mkurugenzi
wa benki ya UBA Tanzania, Mh Peter Makau akichukua pesa katika mashine
ya kutolea pesa ya benki ya UBA Tanzania mara baada ya kuiamuru mashine
huku anayeshuhudia kushoto kwake akiwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Benki hiyo Jenerali Mstaafu, Mh Robert Mboma.
Baadhi
ya wafanyakazi wa benki ya UBA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo kumaliza kuzindua
Mashine hiyo ya UBA Bank, uzinduzi uliofanyika leo Mbezi chini katika
kituo cha mafuta cha Oilcom.
Mkurugenzi
wa benki ya UBA Tanzania, Mh Peter Makau akiongea na waandishi wa
habari mara baada ya mwenyekiti wa bodi ya benki ya UBA Tanzania
Jenerali Mstaafu Robert Mbona kumaliza kuzindua mashine hizo.Picha zote
na Josephat Lukaza
Mwenyekiti
wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya UBA Tanzania, Jenerali Mstaafu,
Robert Mboma leo amezindua mashine nne za kutolea pesa za benki ya UBA
katika kituo cha Mbezi chini huku uzinduzi huo ukiwa ishara ya kuzindua
mashine nyingine tatu zinazopatikana katika maeneo ya Oilcom Mabibo,
Oilcom Segerea, Oilcom Mbezi chini na Oilcom Mkuki Mall ambayo
inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.
Uzinduzi
wa mashine hizi umeenda sambamba na malengo ya benki hiyo ya
kuhakikisha katika ukuaji wake inawasogezea huduma karibu wateja wake.
Akielezea
katika UZinduzi huo Mkurugenzi wa Benki hiyo Hapa Tanzania, Mh Peter
Makau amesema kuwa UBA benki ilikua na ndoto ya kusogeza karibu huduma
zake huku lengo lao likiwa ni kuwa na mashine za kutolea pesa nje ya
matawi yake na kwa kuanza tumeanza na Mashine za ATM nne ambazo zipo
kwenye maeneo muhimu kama vile Oilcom Mabibo, Oilcom Segerea, Oilcom
Mbezi chini na nyingine ndani ya jengo la manunuzi la Mkuki ambalo
litafunguliwa hivi karibuni.
Vilevile
Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo amesema kuwa aliruhusu kuanzishwa kwa
mashine hizo za ATM kwaajili ya kuhakikisha inaendelea kukuza uchumi kwa
Watanzania huku pia wakitarajia kufungua matawi mengine ndani ya
Tanzania hivi karibuni.
Tags
MABENKI