Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.
Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo
cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana
akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya
usiku.
Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea
litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake
wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane
hadharani.
Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya
Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku
mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa
hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi
siuoni.
Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya
hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye
mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.
Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani
kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku
kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa
ushindi wapinzani wake.
Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.
Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.
Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi
mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi
nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.
Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu.
Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila
aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na
Magufuli ni wapenzi....seriously?
Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyonyo zenu? Acheni masikhara bana.
Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.
