BANDA MEDIA BLOG

UONGOZI WA SIMBA UPO TAYARI KWA GHARAMA YOYOTE POINTI SOTE ZA KANDA YA ZIWA


Mzamiru-Yasini-Simba-Bongosoka
Na Carlos Nichombe
UONGOZI wa klabu ya Simba umesema upo tayari kutumia gharama yoyote, ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya timu za kanda ya ziwa ambazo zimekuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu.

Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Kaburu alisema kikosi chao kimekuwa kikipata upinzani mkubwa kutoka kwa klabu za kanda ya ziwa hususani Toto Africa.
Alisema endapo watafanikiwa kuibuka na ushindi katika kanda hiyo watakuwa wamejiweka katika mazingira mazuri ya kuibuka na ubingwa wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara(VPL).
“Najua Simba hatuna rekodi nzuri na timu za kanda ya ziwa hata kama zinakuwa zipo kwenye nafasi mbaya za msimamo wa VPL lakini safari hii hatutakuwa tayari kuona tunapoteza ubingwa kwa sababu yao,”alisema Kaburu.
Aliongeza kuwa Simba inawachezaji mahiri wenye uwezo wa kubadili matokeo ya mchezo wakati wowote ule,tofauti na hapo awali ambapo baadhi ya idara zilikuwa zikionekana kutokuwa makini.
Kaburu alisema mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo waendelee kuwa na imani na wachezaji bora wa kikosi hicho kilichoshindwa kuchukua ubingwa kwa miaka kadhaa.
Pia Kaburu aliongeza kuwa timu yao imejipanga vyema kupambana na kila
kikwazo kitakachokuwa mbele yao kinachotaka kurudisha nyuma jitihada zao za kuchukua pointi tatu muhumi zitakazowasaidia kunyakua ubingwa wa VPL.
Alidai kila idara inayopatikana katika timu hiyo imekwisha kabidhiwa jukumu la kufanya ambalo litawasaidia kutoka na ushindi kwenye michezo yote sita ya VPL ligi iliyosalia kwa timu hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG