Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Josephat Gwajima ametaja makosa ya kisheria yaliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam,Paul Makonda kukimbilia Afrika Kusini.
Akizungumza jana kanisani kwake, Ubungo,
jijini hapa, Gwajima alidai kosa la kwanza la Makonda ni kughushi
cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa
yeye ni Daudi Bashite.
“Kosa hilo kwa mujibu wa Gwajima ni
kifungo cha miaka saba.Kosa jingine ni kula kiapo cha ukuu wa wilaya na
ukuu wa mkoa akisema yeye ni Makonda wakati akijua yeye ni Bashite,”
alisema
Gwajima alisema kosa la hilo la kula kiapo na cheti feki ni kifungo cha miaka mitatu.
Kosa jingine alisema ni kupokea
mshahara na posho kwa jina la Makonda wakati akifahamu si yeye na
kuongeza kuwa kosa hilo likithibitika atatakiwa kurudisha mishahara na
posho zote alizochukua.
Tags
HABARI ZA DINI
