Alhamis
,Machi 16,2017 kumefanyika Mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutoka
wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu na wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Mgeni
rasmi katika mkutano huo ulioandaliwa na shirika la OXFAM na asasi isiyo
ya kiserikali inayojishughulisha na Maendeleo ya Jamii (Relief to
Development Society- REDESO) alikuwa mkuu wa wilaya ya Kishapu
mheshimiwa Nyabaganga Talaba.
Awali akizungumza katika mkutano
huo,Mratibu Miradi (uchumi) kutoka shirika la OXFAM Haji Kihwele alisema
lengo la mkutano huo kuwaweka pamoja wadau hao ili waweze kufahamiana
sambamba na kujadili namna ya kulifanya zao hilo kuwa na tija na manufaa
zaidi kwa wakulima na kuwasaidia wakulima hao kupata masoko.
“Tumekutana hapa ili tujadili pia namna ya kumuunganisha mkulima
wa mkonge anufaike na masoko yenye faida na kupata uwakilishi mzuri
katika sekta hii”,alisema Kihwele.
Akizungumza katika mkutano huo,mkuu wa
wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba aliwataka wadau wa zao la
mkonge kwenda kuwekeza kwa kujenga viwanda katika wilaya yake kwani
ardhi ipo ya kutosha.
“Wadau wa mkonge njooni Kishapu
muwekeze,tunayo ardhi ya kutosha,hivi sasa maji kutoka ziwa Victoria
yamefika Kishapu,umeme na barabara zinazopitika kipindi chote
zipo,tunataka kulifanya zao la mkonge kuwa rasmi badala ya kutumika
kwenye mipaka kutenganisha mashamba na milingoti kwa ajili ya kujengea
nyumba”,alieleza Nyabaganga.
“Kipindi cha majaribio
kimekwisha,tunalima pamba lakini pia tumeamua kulima mkonge,tunataka
kilimo hiki kiwe rasmi,wananchi wanajitahidi kulima zao la mkonge lakini
changamoto kubwa iliyopo ni ukosefu wa soko hivyo ni vyema ofisi za
bodi ya mkonge zikawa na ofisi katika maeneo yanayolima,wakulima
wanahitaji kunyanyuliwa kwani hata mikopo inayotolewa haitoshi”,aliongeza Nyabaganga.
Miongoni mwa wadau walioshiriki katika
mkutano huo ni wakulima na wasindikaji wa zao la mkonge,wazalishaji wa
bidhaa za mkonge,taasisi za kifedha ikiwemo Vision Fund,bodi ya mkonge
(TSB),Chemba ya wafanyabiashara,wakulima na viwanda (TTCIA),Shirika la
kuhudumia viwanda vidogo (SIDO),Umoja wa Vikundi vya Wakulima Tanzania
(MVIWATA),Mtandao wa Asasi za Wakulima (Agriculture Non- State Actors
Forum -ANSAF) na viongozi mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya
Kishapu na Meatu.
Tazama picha 26 za matukio yaliyojiri wakati wa mkutano huo
Mratibu Miradi (uchumi) kutoka shirika
la OXFAM Haji Kihwele akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa zao la
mkonge uliofanyika katika ukumbi wa Virgimark Hotel mjini Shinyanga leo
Alhamis Machi 16,2017-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Wadau wa zao la mkonge wakimsikiliza Mratibu Miradi Kiuchumi kutoka OXFAM Haji Kihwele
Meneja Mradi wa asasi isiyo ya
kiserikali inayojishughulisha na maendeleo ya jamii (Relief to
Development Society- REDESO) Charles Buregeya akizungumza katika mkutano
wa wadau wa zao la mkonge kutok wilaya ya Kishapu na Meatu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga mheshimiwa Nyabaganga Talaba akizungumza wakati wa mkutano huo
Washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa
Nyabaganga Talaba akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la mkonge
kutoka wilaya ya Meatu na Kishapu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba akizungumza ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa
Nyabaganga Talaba akizungumza ukumbini ambapo alisema serikali
imedhamiria kuanzisha viwanda na kwamba kinachotakiwa ni kuwa tayari
kuzalisha zao la mkonge.Kulia ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Kishapu George Kessy
Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo na Afisa Biashara halmashauri ya
wilaya ya Kishapu Konisaga Mwafongo
Mratibu wa Miradi (Ardhi) kutoka OXFAM bi Amina Ndiko akisisitiza jambo kwenye mkutano huo
Meneja Mradi REDESO Charles Buregeya (kushoto) na Mratibu Miradi (uchumi) shirika la OXFAM Haji Kihwele
Mratibu wa Miradi (Ardhi) kutoka OXFAM bi Amina Ndiko akizungumza ukumbini
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo akichangia hoja katika mkutano wa wadau wa zao la mkonge
Mwakilishi wa Shirikisho la Wakulima na
Wasindikaji wa zao la mkonge wilaya ya Kishapu( SHIWAKI),Yusuph Mboje
akielezea kuhusu kazi zinazofanywa na shirikisho hilo lililoanzishwa
mwaka 2016 ambalo linakabiliwa na changamoto ya kukosa soko la mkonge na
kukosekana kwa mkataba na mnunuzi wa kudumu wa zao hilo
Mwakilishi wa akina mama
wanaojishughulisha na kilimo cha mkonge Anastazia Christopher kutoka
Kishapu akielezea faida wanazozipata kupitia kilimo cha mkonge ambazo ni
pamoja kuacha kuwa tegemezi kwa waume zao,kusomesha watoto n.k
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo na mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba wakiwa ukumbini
Mratibu wa Miradi (Ardhi) kutoka OXFAM bi Amina Ndiko akiongezea maelezo kutoka kwa akina mama kutoka Kishapu wanaolima mkonge
Mkulima wa zao la mkonge kutoka Kishapu
Fredina Said akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Nyabaganga Talaba
zulia lililotengenezwa kwa mkonge
Mraghbishi kutoka Taasisi ya Kuimarisha
Demokrasia na Utawala Bora (ADLG) ambaye pia ni Mwakilishi wa Mtandao wa
Asasi za Wakulima (Agriculture Non- State Actors Forum -ANSAF) bwana
Nicholaus Luhende Ngelela akizungumza kwenye mkutano huo ambapo
alisisitiza umuhimu wa wakulima wa zao la mkonge kuunda mtandao wao
Katibu mtendaji Chemba ya wafanyabiashara,wakulima na viwanda (TTCIA) mkoa wa Mwanza Hassan Karambi akizungumza ukumbini
Taasisi isiyo ya kiserikali yenye
kusaidia sekta ya kilimo (Private Agricultural Sector Support – PASS)
Emilian Barongo akizungumza ukumbini
Jeremiah Maleko kutoka Vision Fund akieleza namna wanavyotoa mikopo kwa wakulima
Afisa
udhibiti Ubora kutoka Bodi ya Mkonge Olivo Mtunge akielezea kuhusu hali
ya soko la mkonge hivi sasa na fursa za mkulima mdogo ili aweze
kunufaika na kilimo hicho
Picha ya pamoja washiriki wa mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutoka wilaya ya Meatu na Kishapu
Picha ya pamoja washiriki wa mkutano huo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Tags
MIFUGO/KILIMO/UVUVI