Mratibu wa Mradi wa SPANEST
nchini, Godwell Meing’ataki (kushoto) akiteta neno na mgeni rasmi
Katibu Tawala mkoa wa Njombe, Jackson Saitabau mara alipowasili kuja
kufungua mafunzo ya muda siku tatu kwa washiriki 90 katika fani ya
Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na
SPANEST yanayofanyika Mkoani Njombe
Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya
Utalii, Paskas Mwiru alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi, Katibu Tawala
wa mkoa wa Njombe kufungua mafunzo hayo jana katika fani ya Utalii na
Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST
yanayofanyika Mkoani Njombe kwa muda wa siku tatu na yakiwa na jumla ya
washiriki 90. Katikati ni Katibu tawala wa Mkoa wa Njombe pamoja na
Mratibu wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki (Picha na Lusungu
Helela- WMU)
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe,
Jackson Saitabau akizungumza na jumla ya washiriki 90 wakati alipokuwa
akifungua jana mafunzo ya fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na
Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yanayofanyika Mkoani Njombe kwa
muda wa siku tatu. na Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini,
Godwell Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii,
Paskas Mwiru (kulia)
Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa
cha Utalii,Jesca William akiwaelezea washiriki wa mafunzo kusoma kozi
zinazotolewa na Chuo cha Taifa cha Utalii mara baada ya mgeni rasmi
kufungua mafunzo ya siku tatu katika fani ya Utalii na Ukarimu
yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yanayofanyika
Mkoani Njombe.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe,
Jackson Saitabau akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua
mafunzo ya jumla ya wahudumu 90 wa Hoteli, Migahawa na Nyumba za
kulala wageni mkoani Njombe watakaopewa mafunzo ya siku tatu katika
maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na
upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu. Mafunzo hayo yameandaliwa na
Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST , lengo likiwa ni kuongeza
ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta hiyo ili kukidhi mahitaji ya
soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya
kiwango. Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell
Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskas
Mwiru (kulia)
Mratibu wa Mradi wa SPANEST
nchini, Godwell Meing’ataki akizungumza na vyombo vya habari mara baada
ya mgeni rasmi kufungua mafunzo ya muda siku tatu kwa washiriki 90
katika fani ya Utalii na Ukarimu
Mmoja wa Washiriki wa mafunzo
katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja
na upishi katika fani ya Utalii na akielezea jambo kwa Mkufunzi wa Chuo
cha Taifa cha Utalii, Dawson Kyungai mara baada ya Mgeni rasmi kufungua
mafunzo katika fani ya ukarimu na Utalii.
………………………………………………………………………..
Serikali kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Mradi wa SPANEST imeanza
jitihada za kuinua na kuendeleza Utalii kwa mikoa ya Nyanda za Juu
Kusini kwa kuanza kutoa mafunzo katika sekta ya ukarimu na utalii kwa
wahudumu 90 wa hoteli, migahawa na nyumba za kulala wageni ili
kuwawezesha kutoa huduma zenye hadhi kwa watalii.
Kufuatia hali hiyo, wahudumu hao
wameanza kupewa mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya
chakula na vinywaji pamoja na upishi kwa lengo likiwa ni kuongeza ubora
wa huduma zinazotolewa katika sekta ya ukarimu na utalii ili kukidhi
mahitaji ya soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo
chini ya kiwango kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini
Hayo aliyasema jana na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Njombe, Jackson Saitabau wakati alipokuwa akifungua
mafunzo ya ukarimu na utalii kwa jumla ya washiriki 90 yanayofanyika kwa
muda wa siku tatu mkoani Njombe na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
kushirikiana Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
kupitia Mradi wa SPANEST unaotekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA).
Aliongeza kuwa licha ya ukanda
huo kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini idadi ya watalii imezidi
kuwa ndogo, Hivyo mafunzo hayo watakayoyapata yatakuwa chachu katika
kukuza na kuendeleza utalii kwa kutoa huduma zenye viwango kwa watalii
pindi wanapokuja kutembelea vivutio vya utalii.
Saitabau amewataka wahudumu
waache tabia ya uvivu na kufanya kazi kwa mazoea pindi wanapotoa huduma
kwa watalii kwa kuwa wanaoharibu sifa ya Mkoa na kuwataka mafunzo
watakayopata yawe chachu katika kukuza na kuendeleza utalii.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Utalii, Paskas Mwiru amesema mafunzo hayo hayataishia kwa watoa huduma
tu katika hoteli pia mafunzo hayo yataendeshwa kwa wamiliki wa sehemu
hizo ili waweze kuwalipa malipo stahiki wafanyakazi wao wanaofanya kazi
katika sehemu hizo.
Kwa Upande wa Mratibu wa Mradi wa
SPANEST, Godwell Meing’ataki amesema mafunzo hayo yanafanyika ili
kuwawezesha wahudumu kuwa na ujasiri na kujiamini pale wanapotoa huduma
kwa watalii.
‘’ Sisi tunaamini tukiwapa ujuzi
wahudumu hawa tutakuwa tumefungua milango ya watalii wengi zaidi kuja
kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Nyanda za Juu kusini’’ alisema
Meing’ataki
Hadi hivi sasa mafunzo
yameshafanyika mkoani Mbeya na kwa sasa yanafanyika Njombe baada ya hapo
yatafanyika Iringa na hatimaye mkoani Songwe
Tags
MALIASILI/UTALII