BANDA MEDIA BLOG

WAKAZI WA MTAA WA SENJE KATA YA MSALATO DODOMA, WAISHANGAA TAARIFA YA HALMASAHAURI KUONYESHA KUWA BARABARA YAO IMECHONGWA WAKATI HAIJAWAHIHI KUGUSWA TANGU MWAKA 1979

Gari likipita kwenye dimbwi la maji ambalo lipo katika barabara ya mtaa wa senje kata ya msalato ambapo Dimbwi hilo husababisha adha kubwa kwa wakazi wa mtaa huo kutokana na kushindwa kupita kwa miguu au vyombo vya usafiri hasa kipindi cha mvua

Watoto wakitafuta uwezekano wa kupita katika eneo hilo ambalo kwa asili ni eneo lenye tope jingi

Diwani wa kata ya Msalato Ally Mdende Mohamed akizungumza na wakazi wa mtaa wa senje waliokusanyika katika barabara hiyo ili kupata majibu toka kwa diwani huyo kuwa ni lini itachongwa na kujengewa daraja  [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]




WAKAZI wa mtaa wa senje kata ya msalato manispaa ya Dodoma wameshangazwa na taarifa ya matengenezo ya barabara yenye ulefu wa km 1 katika mtaa wao toka manispaa huku wao wakiendelea kupata adha ya kushindwa kuitumia katika misimu yote ya mvua kutokana na ubovu
Akiongea na waandishi wa habari mzee Yona Mkuki ambae ni mkazi wa miaka mingi katika mtaa huo alisema kuwa Barabara hiyo haijawahi kuonja greda tangu mwaka 1979 ilipochongwa na jeshi.
Mkuki alisema baada ya hapo hakujawa na chombo au mtu toka manispaa aliyefika na kufanya matengenezo yoyote pamaoja na kuwa kila mtu anajua adha wanayoipata ya magari kushindwa kupita hali inayowasababishia wagonjwa kutembea kwa miguu na wengine kubebwa migoni mpaka kufika kuliko na unafuu
“taarifa ya barabara hii kutengenezwa mwaka jana ndiyo nazisikia sasa hivi labda kama kule ofisini na kwenye makaratasi yao lakini kiuhalisia tunapata adha kubwa kutokana na mashimo yanayosabisha maji kutuama tena kukiwa na tope jingi wakati wa mvua
Mwaka jana sina niliyemuona wala greda bali ninachojua barabara hii ilitengenezwa na jeshi mwaka 1979 alisema”,
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Msalato Ally Mdende Mohamed alisema mwanzoni mwa mwaka 2016 aliomba kutengenezewa barabara hiyo na baadae ikaingizwa kwenye mpango wa kutengenezwa baada ya mhandisi kufanya savei
Diwani huyo alisema kuwa kilichomshangaza ni mwezi octoba mwaka jana kuona kwenye makablasha kuwa barabara hiyo ilishatengenezwa na mkandarasi Alishalipwa fedha yote  zaidi ya 8.6 mil
“Hii ni ajali niliyokuwa nimetegeshewa ili nije kuonekana kuwa nimepewa fedha na kuzila mimi na huyo mkandarasi kitu ambacho mimi sikuhusika
Aidha alisema kablasha linaonyesha kuwa barabara hiyo imechongwa na kushindiliwa, karavati limejengwa, vichaka vimefyekwa na visiki kung’olewa kitu ambacho siyo cha kweli  

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG