baadhi ya nyumba zilizopo Mpigi
darajani ambazo zinatakiwa kubomolewa kutokana na kujengwa ndani ya mita
sitini kutoka katika chanzo cha maji. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) amegiza
wenye nyumba hizo wabomoe kwa gharama zao wenye.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) akiongea na
wananchi wa eneo la Mpigi darajani (hawapo pichani) na kusisitiza katazo
la kufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita sitini. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Bi. Fatuma Latu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) alipotembelea
Mamlaka ya Usafi na Mazingira Chalinze kujionea changamoto za uchafuzi
wa mazingira katika mto Wami
……………….
Na Lulu Mussa
Bagamoyo – Pwani
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameagiza kusitishwa
mara moja kwa shughuli zote za kibinadamu kando kando ya Vyanzo vya
maji.
Rai hii imetolewa leo na Waziri
Makamba mara baada ya kufanya ziara ya kukagua hali ya mazingira katika
Mkoa wa Pwani eneo la Mto Mpiji ambao umeathirika kutokana na Uchimbaji
wa mchanga na mmomonyoko wa ardhi unaohatarisha maisha ya wakazi wa eneo
hilo.
Waziri Makamba amemuagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Bi. Fatuma Latu kuwaondoa watu
wote waliojenga pembezoni mwa Mto Mpiji na kuhakikisha zoezi hilo
linafanyika ndani ya siku 30. ” Mkurugenzi hakikisheni kuwa wakazi hao
waliovamia eneo la mto huu na kujenga makazi yao ya kudumu wanaondolewa
mara moja” Alisisitiza Waziri Makamba.
Katika hatua nyingine Waziri
Makamba ametembelea Mto Wami na kusikitishwa na uharibifu mkubwa wa
mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na
kilimo, ufugaji na uchimbaji haramu wa madini, upasuaji mbao na uchomaji
mkaa unaopelekea mmomonyoko wa udongo na mchafuko/tope jingi na
kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa maji.
Katika kukabiliana na changamoto
zilizoainishwa Waziri Makamba amesema Ofisi yake itaanda kikao kazi
kitakachojumuisha wadau wote muhimu ili kunusuru Mto Wami haraka
iwezekanavyo. “Serikali haiwezi kuwekaza fedha nyingi kwenye mradi
mkubwa kama huu na kuona uharibifu ukiendelea na kuharibu miundombinu,
hali hii haikubaliki na nitachukua hatua za haraka.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) yuko katika
ziara ya kikazi katika mikoa Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara
na Singida kujionea hali ya mazingira na changamoto za hifadhi katika
mikoa husika. Hii ni ziara ya pili baada ya iliyofanyika mwezi Oktoba
2016, katika mikoa ya Nyanda za juu Kusini. Katika siku ya kwanza Waziri
Makamba ametembelea Mto Mpigi, Mto wami na hifadhi ya msitu wa Kibindu
uliovamiwa na wananchi.
Tags
WALIOJENGA MABONDENI