BANDA MEDIA BLOG

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MALI YA KALE ILI KUIMARISHA UTALII NCHINI


images
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali imewataka Wananchi kushiriki Kutunza Mali Kale kwa Faida ya Kizazi hiki na Kizazi kijacho ili ziweze kuchangia katika Kukuza Uchumi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mambo ya Kale toka Wizara ya Mali Asili na Utalii Dkt. Donatius Kamamba wakati wa mkutano na waandishi wa habari  uliolenga  kuhamasisha wananchi kutumia fursa zinazotokana na uwepo wa mali kale. leo Jijini Dar es Salaam.
“Mali Kale ni kichocheo cha Utalii na ukuaji wa Uchumi hapa nchini hivyo ni muhimu zikatunzwa na kuenziwa ili ziweze kusaidia Taifa kukuza sekta ya Utalii nchini” Alisisitiza Dkt. Kamamba.
Akifafanua zaidi Dkt. Kamamba amesema kuwa Mali kale ni urithi wa taifa na sekta hiyo imekuwa ikichochea Tafiti,machapisho na makala simulizi hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya elimu na uchumi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Msaidizi utafiti Dkt.Emmanuel Bwasiri amesema kuwa mali kale  ni utambulisho wa taifa letu hivyo ni muhimu kusaidia katika kutunza rasilimali hizo ambazo zinasaidia kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi.
Akizungumzia vigezo vinavyotumika kutangaza eneo kuwa urithi wa taifa Dkt Bwasiri amesema kuwa ni Sifa ya Kiuchumi,Kijamii,Kielimu na Kihistoria.
Serikali imekuwa ikisisitiza utunzanji wa Mali kale katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili ziweze kuchochea ukuaji wa uchumi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG